Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akitoa taarifa kwa wanahabari leo katika ofisi za jeshi hilo mkoa. |
Na Walter Mguluchuma,Katavi
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ernest Lyoba (61) Mkazi wa Kijiji cha Namanyere Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele amejeruhiwa vibaya katika sehemu yake ya uso na mgongoni baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasio julikana wakati akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake.
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Ernest Lyoba (61) Mkazi wa Kijiji cha Namanyere Kata ya Majimoto Wilaya ya Mlele amejeruhiwa vibaya katika sehemu yake ya uso na mgongoni baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasio julikana wakati akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani amewaambia wandishi
wa habari kuwa tukio hilo la kikatili la kusitishia
limetokea June 25 huko katika eneo la Kijiji cha
Namanyere.
Amebainisha
kuwa siku ya tukio mhanga alikuwa yuko
njiani akiwa anaelekea nyumbani kwake
majira ya saa tisa alisiri mara baada ya kuwa
amemaliza shughuli zake za kujitafutia riziki ndipo watu wasio julikana
walimmwagia tindikali sehemu za usoni na mgongoni na kumjeruhi
vibaya na kisha watu hao walitokomea mahali pasipo julikana .
Kamanda
Ngonyani amesema baada ya mhanga kuwa amemwagiwa tindikali
hiyo alipiga kelele za kuomba msaada na baada ya muda mfupi watu
walifika kwenye eneo hilo na kumkuta Ernest Lyoba akiwa
amejerihiwa vibaya .
Ameeleza
wasamalia hao wema walimchukua mhanga huyo na kumkimbiza kwa haraka
hadi kwenye Hospitali ya Halmashauri ya
Mpimbwe kwa ajiri ya matibabu hata hivyo kutokana na kuwa
amejeruhiwa vibaya mhanga alipewa rufaa ya kwenda
kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi .
Hata hivyo
baada ya kuwa amefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Katavi alipewa tena ya kwenda kupatiwa matibabu
zaidi kwenye Hospitali ya Rufaa ya KMC ya
Mkoani Kilimanjaro ambako amelezwa hadi sasa.
Kamanda
Ngonyani amesema juhudi za kuwasa watuhumiwa hao
zinaendelea kufanywa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi ili kuhakikisha
linawakamata nakuwa tia nguvuni na kuwafikisha mara moja
Mahakamani ili wakajibu mashitaka ya tuhuma zitakazo
kuwa zinawakabili.