Na Walter
Mguluchuma,Katavi .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewahakikishia wananchi wa Mkoa huu kusherekea sherehe za EID AL HAJJ k wa Amani na utulivu kutoka na jeshi hili lilivyojipanga na walivyoimarishaulinzi wakati wa kipindi cha sikukuu na baada ya sikukuu katika kuhakikisha Mkoa wa Katavi unaendelea kuwa salama.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limewahakikishia wananchi wa Mkoa huu kusherekea sherehe za EID AL HAJJ k wa Amani na utulivu kutoka na jeshi hili lilivyojipanga na walivyoimarishaulinzi wakati wa kipindi cha sikukuu na baada ya sikukuu katika kuhakikisha Mkoa wa Katavi unaendelea kuwa salama .
Kaulu hiyo ya jeshi la polisi Mkoa wa Katavi
imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster
Ngonyani wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa Habari ofisini
kwake .
Amesema Jeshi la Polisi Mkoa
wa Katavi linawahakikishia wananchi wa Mkoa huu kuwa wamejipanga
ipasavyo kuhakikisha wakati wa kipindi cha sikukuu ya EID
AL HAJJ na baada ya sikukuu Amani na utulivu katika Mkoa wa
Katavi inaendelea kuwepo .
Ameeleza kuwa wakati wa sikukuu wananchi
wawe na Amani katika kusherkea sikukuu hiyo
kwa usalama kwani polisi wamejipanga kufanya doria mbalimbali
kwenye maeneo yote ya Mkoa huu na kwenye barabara zinazo toka na
kuingia ndani ya mkoa .
Kwani muda wote watakuwa wanazunguka kwa kufanya doria za
miguu , gari pikipiki kwenye maeneo yote hivyo kama kutakuwa
na tukio lolole na kuta kuwepo kwa viashiria vya uvunjwaji wa Amani
wananchi watowe taarifa mara moja ili hatua za haraka ziweze
kuchukuliwa .
Aidha jeshi la polisi limeweza
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na Televisheni
tatu inchi 42 aina ya Philips ,Hisense
inchi 43 Televisheni aina ya Samsang inchi 43.
Kamanda Kaster Ngonyani ametaja mali
nyingine walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni Radio sabusa
moja aina ya seapiano na baiskeli
moja aina ya ngamia mali hizo zote zinazosadikiwa kuwa ni za
wizi wamekamatwa nazo wakiwa wamezificha ndani ya nyumba zao wanazo ishi.
Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Hassan Ramadhan
na Vicent Ndika wote wakazi wa Mtaa wa
Kwalakwacha Nsemlwa ambapo jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linaendelea
kuwashikilia watuhumiwa hao
Kamanda Ngonyani anatowa wito kwa wananchi walioibiwa mali za aina hiyo kufika katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda wakiwa na risiti zenye kuonyesha uhalali wa kuzitambua mali hizo.