WATUHUMIWA 34 WAKAMATWA KWA MAKOSA MBALIMBALI YA UHALIFU KATAVI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani akizungumnza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu taarifa mbalimbali za uhalifu.

Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 kwa tuhuma  za matukio mbalimbali  ya uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januari  wakiwemo watuhumiwa watatu waliokamatwa wakiwa na  meno ya Tembo  tisa  na vipande  tisa ya nyama  tembo pamoja na  bunduki moja  aina ya shortgun.
Jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 34 kwa tuhuma  za matukio mbalimbali  ya uhalifu kwa kipindi cha mwezi Januari  wakiwemo watuhumiwa watatu waliokamatwa wakiwa na  meno ya Tembo  tisa  na vipande  tisa ya nyama  tembo pamoja na  bunduki moja  aina ya shortgun.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi   Kaster Ngonyani amewaambia wandishi wa Habari watuhumiwa hao wa uhalifu wamekamatwa kufatia msako mkali unao uendelea  kufanywa na jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huu wa kuwasaka watu wote wanao  jihusisha na matukio ya uhalifu .

Amesema watuhumiwa hao  34 wamekamatwa katika kipindi cha mwezi januari 2026 katika watuhumiwa hao 3  wamekamatwa wakiwa na nyaraza Serikali meno  sita ya tembo  nyama ya  pori Tembo  kilo 71, watuhumiwa 9 wamekatwa wakiwa na  bunduki aina ya gobore   8 na risasi zake 63 na shortgun moja  na risasi 12 watuhumiwa hao  wamekuwa wakijihusisha na uwindaji haramu wa  wanyama pori.

Kamanda Ngonyani amesema katika msako wamefanikiwa pia  kuwakamata watuhumiwa 8 wakiwa  na  dawa za kulevya  aina ya  Bangi  kilo  70  na kete 320 pia watuhumiwa watatu  wamekamatwa  wakiwa na noti  bandia 10 za dola 100 na noti 323 za tshs zote zikiwa  na namba moja  DF 5893401.

Kwa  upande wa makosa  ya usalama  barabarani   kwa  kipindi  hicho cha mwezi  wamefanikiwa  kukamata makosa  2,351 ya ukiukwaji  wa sheria  za usalama barabarani  ikiwa ni katika jitihada zinazo endelee kufanywa na jeshi hilo  za  kuzuia  ajari za barabarani .

Kamanda Ngonyani ametowa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Katavi  kuacha tabia ya kujihusisha  na vitendo vya uhalifu  kwani  kufanya hivyo watambue kuwa wataishia mikononi mwa jeshi la polisi ambao muda wote wapo kazini.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages