Meneja wa Benki ya CRDB benki akizungumnza na wanawake na Vijana wajasiliamali wakati wa kutambulisha fursa ya utoaji wa Mikopo kwa wanawake na vijana inayo julikana kama IMBEJU. |
Wanawake na vijana Wajasiliamali katika Mkoa wa Katavi wameobwa kuwa waaminifu katika kurejesha fedha wanazopatiwa na Benki ya CRDB ili kuendelea kukuza Biashara yao kuptia mikopo hiyo nafuu inayotolewa na Benki hiyo.
Msitahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry akifungua hafla ya utambulisho wa huduma ya utoaji Mikopo kwa wanawake na Vijana Chini ya Benki ya CRDB benki |
Wanawake na vijana Wajasiliamali katika Mkoa wa Katavi wameobwa kuwa waaminifu katika kurejesha fedha wanazopatiwa na Benki ya CRDB ili kuendelea kukuza Biashara yao kuptia mikopo hiyo nafuu inayotolewa na Benki hiyo.
Wito huo umetolewa na Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Sumry wakati wa Hafla ya kutambulisha Fursa
ya utoaji wa Mikopo kwa Vijana na wanawake inayotolewa na Benki ya CRDB inayojulikana kama IMBEJU.
‘’niendelee kusisitiza uaminifu
uadilifu ndio kitupekee ambacho kinaweza kutuondelea changamoto hizi za ukosefu
wa Mitaji tukiwaa waaminifu Benki itaendelea kutushika Mkono wakikuona wewe
unafanya vizuri kwenye Mokopo huu wataweza kukuweka kwenye mikopo mikubwa ‘’amesema
sumry
Amesema fursa hiyo ya utoaji wa
mikopo kwa wanawake na vijana wajasiliamali isiyo kuwa na Dhamana wala Riba Masahrti
Magumu itapunguza malalamiko kwa wanawake ambao wamekuwa wakipata changamoto ya
liba Kubwa kwenye taasisi za fedha za mitaani maalufu kama mikopo umiza.
‘’nimekuwa nikipokea malalamiko
mengi kwa akina mama wajasiliamali hasa wa Mpanda wamekuwa wakilalamikia sana
hizi taasisi zinazo toa mikopo chechefu fursa hii ya IMBEJU kupitia CRDB Benki inakuja kutatua changamoto hizo za utoaji
wa mikopo chechefu kwa wajasiliamali’’
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la
Mpanda Mohamed Masood amesema Benki hiyo imekuja na mpango na Huduma ya IMBEJU
Kwa kutoa mikopo kwa vijana na wanawake wajasiliamli pasipo na Riba wala
dhamana kwa masharti ya kuwa na biashara yeyote inayoonekana.
‘’hapa tunazungumzia IMBEJU
maana yake ni mtaji wezeshi ambao utatolewa kwa wajasiliamali wadogo waliopo
katika vikundi lakini haina maana kwamba tutatoa kwa kikundi tutatoa kwa
mwanakikundi mmoja mmoja kwa sharti la kuwa mwanakikundi’’
Ameeleza kuwa utoaji wa mikopo
hiyo kwa vijana na wanawake wajasiliamli utazingatia uhai wa Biashara
inayofanyika kulingana na mahitaji ya
biashara husika kwa lengo la kuendelea kukuza biashara hiyo.
‘’Kama wewe ni Mfinyazi
tutaangalia biashara yako hiyo kama wewe unatengeneza vikapu unauza matunda tutaangalia
uwezo wako wa kufanya Biashara lakini ni kiasi gani biashara yako inataka ili
iweze kukua’’ amesema Masoudy
Katika hatua nyingine amsema
kuwa fursa hiyo itakuwa na uwezo kwa mnufaika kuwa na Akaunti maalumu ya Benki
ya CRDB kwaajili ya Huduma hiyo ya IMBEJU
Monica Yusuph moja ya wanawake
walishiriki katika hafla hiyo anasema ‘’tumeona kwamba mnatujali hata sisi wajasiliamali
wadogo kupitia mikopo hii inaonyesha isahara ya kulijenga taifa kwa pamoja
hongrereni sana CRDB Benki ‘’
Kwa upande wake Herena pascha
amesema kuwa amefurahishwa na mpango huo wa CRDB benki kuja na Huduma ya IMBEJU
itawasaidia kwakuwa haina Riba wala dhamana kwenye ukopaji wake.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com