Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Wanawake Mkoa wa Katavi wameelezwa kuwa wanaweza kuzuia magonjwa ya
mlipuko ya kuarisha kwa watoto wachanga kwa kuwanyonyesha maziwa pekee
ndani ya mienzi sita tangu kuzaliwa kwani imedhibitishwa kisayasi kuwa maziwa
ya mama yanavirutubisho vyote kwa asilimia mia moja.
Mratibu wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko wa Hosptali teule ya
rufaa ya Mkoa wa Katavib Dkt Taphinez Machibya akizungumza jana ofini kwake na
waadishi wa habari alisema kuwa kunyonyesha,kuhakikisha mitindo mizuri ya
usafi,uchanjaji (hasa dhidi ya virusi vya rota na surua) na kuhakikisha chakula
ni salama itasaidia watoto wachanga kuepukana na magonjwa ya kuharisha.
Dkt Machibya alibainisha kuwa kuharisha kwa watoto wadogo ni tatizo
linaloshika nafasi ya pili duniani kwa kusababisha vifo miongoni mwa watoto
chini ya miaka mitano wanaofariki,mmoja hufa kwa sababu ya kuharisha.
Alieleza kuwa sababu ya kuharisha kwa watoto kunaweza kusababishwa na
aina mbalimbali za vimelea ingawa kunaweza kusitokane na maambukizi ya vimelea
(non-infectioud causes).
Vimelea vinavyosababisha kuharisha ni virusi vinaogoza katika
kusababisha tatizo la ugonjwa wa mlipuko wa kuharisha kwa watoto katika nchi
zinazoendelea,Bakteria nao wanasababisha kuharisha kwa asimilia 2-10 ambapo
husababishwa na upotevu mdogo wa maji ukilinganishwa na virusi.
Aidha Parasite husababisha ugonjwa wa mlipuko wa kuharisha kwa watoto
lakini aina hii huwa ni sugu zaidi (chronic diarrhea) ambapo mara nyingi
huambatana na homa,kutapika,upugufu wa maji mwilini.
Dkt Machibya alifafanua baadhi ya dalili za ugonjwa mlipuko wa kuharisha
kwa watoto kuwa ni watoto wanaohara huwa na dalili kuu tatu ambazo ni
homa,kutapika na kuharisha,Kwa kawaida choo kinakuwa cha majimaji sana.
“ndugu wanahabari dalili hizi zinaonesha kupitia tafiti kuwa asilimia 63
ya watoto wanaolazwa hosptalini kwa tatizo hili wanaonesha dalili zote 3
,aslimia 25 wanakuwa na dalili 2 tu” alisema Dkt Machibya.
Hivyo aliwashauri wanawake kuchuguza kiasi cha maji kilichopotea ,iwapo
uzito wa mtoto utakuwa umepugua kwa zaidi ya asilimia 10 ambapo mtoto atakuwa
na badhi ya dalili za kupoteza fahamu,mapigo ya moyo kwenda kasi,kushindwa
kula/kunyonya,kushindwa kutoa mkojo,kiu na kunywa maji haraka.
Pamoja na hayo aliongeza kuwa namna ya kuzuia maambukizi ni
kuzingatia usafi wa chakula(kupika na kuhifadhi),kunawa mikono kila na baada ya
kutoka chooni,kuwa na makini na watoto wanaoharisha ikiwezekana kuwatenga na
wenzao pamoja na chanjo ya rotavirus.
Nao baadhi ya wanawake mkoani Katavi Elizabeth Kiula alisema kuwa
ugonjwa wa karisha kwa watoto wamekuwa wakiamini unasababishwa na kuhalibika
pekee kwa maziwa ya mama,Hivyo huathri afya ya mtoto baada ya kunyonya.
Vilevile alisema kuwa kuharisha kwa watoto kunatokana na uchafu wa
kupindukia kwa wanawake wakati wa kunyonyesha,Hivyo aliwaomba wanawake wote
kuzingatia masuala ya usafi kwa ajili ya watoto wao.
Esther Baraka alieleza kuwa licha ya juhudi kubwa zinafanywa za
kutokomeza ugonjwa huo wa mlipuko kwa watoto ni vizuri zaidi ikazidi kutoa
elimu kwa makudi yote pamoja na akinababa.
Alisema kuwa jukumu la kuelea watoto nila baba na mama hivyo
wanaposhirikishwa na akinababa itasaidia kutambua jukumu la kuwakinga watoto
dhifi ya magonjwa ya mlipuko.