Wananchi wa Kata ya shanwe na Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
Na Paul Mathias -Katavi
Serikali katika Mkoa wa Katavi
kupitia Wizara ya Maji imeletafedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 kwaajili ya
kuwalipa fidia wananachi 568 wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda watakao pisha
Mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa kupitia chanzo cha maji cha bwawa la
milala.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko akizungumnza na wananchi wanaopisha mradi wa Maji Manispaa ya Mpanda |
Serikali katika Mkoa wa Katavi kupitia Wizara ya Maji imeletafedha kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 kwaajili ya kuwalipa fidia wananachi 568 wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda watakao pisha Mradi wa maji wa miji 28 unaotekelezwa kupitia chanzo cha maji cha bwawa la milala.
Akizungumnza na wananchi wa Mtaa
wa Kigamboni,Shamwe na Mtemi beda zilizopo kata ya Shanwe na Misunkumilo
Manispa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
amesema fedha hiyo tayari imeshafika Mkoa wa Katavi kwaajili ya kuanza
kulipafidia hiyo.
‘’ndungu wananachi jambo letu
limetiki ambalo tulikuwa tunalisubiria kwa hamu sana naomba kuwapa taarifa kuwa
tayari fedha hiyo kiasai cha Shilingi Bilioni 2.9 zimeshafika mkoa wa Katavi
kwaajili ya fidia yenu’’-Mrindoko
Aidha ametoa siku 90 baada ya
Malipo hayo kufanyika kuondoka kwenye maeneo hayo ili serikali iendelee na
ujenzi wa mradi huo wa maji ambao utakuwa mkombozi kwa upatikanaji wa huduma ya
maji kwa wananachi wa Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla.
‘’Nimekubali ombi lenu ya kupeana
siku 90 tangu malipo kufanyika kuhakikisha mnaachia maeneo haya kwakuwa tayari
fidia mtakuwa mmelipwa’’-Mrindoko.
Amewaomba wananachi hao pindi
watakapolipwa fidia hiyo kwenda kufanya kazi za maendeleo kwenye familia zao na
sio kwenda kutumia fedha hizo katika mambo ambayo hayana tija kwao.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta akitoa shukrani kwa serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha kwaajili ya malipo ya fidia kwa wananchi hao. |
Idd Kimanta Mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi [CCM] Mkoa wa Katavi amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Katavi
kuhakikisha malipo hayo yanaanza kufanyika ndani ya wiki mbili ili wanananchi
hao waanze kuandaa makazi yao ya kudumu.
Paul Matyampula Mwananchi mnufaika wa fidia hiyo akitoa neno kwa serikali kwa kusikia kilio cha cha kupatiwa fedha ya fidia |
Mradi wa maji wa Miji 28
unatekelezwa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya
maji kwa kushirikiana na serikali ya India ambapo katika manispaa ya Mpanda
mradi huo utakamilika kwa gharama ya shilingi Bilioni 22.