Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,SACP Kaster Ngonyani akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Jeshi hilo kwa kipindi cha Mwezi Oktoba 2024 kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Katavi. |
Na Paul Mathias-Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa
kuwakamata wahamiaji haramu 14 kutoka nchi za Ethiopia,Burundi na Jamhuri ya
kidemocrasia ya Congo.
Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 14 kutoka nchi za Ethiopia,Burundi na Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Akitoa taarifa ya utendaji kazi
wa Jeshi la Polisi kwa kipindi cha mwezi Oktoba 2024 kwa waandishi wa habari
Mkoa wa Katavi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi SACP Kaster Ngonyani amesema
wahamiaji hao wameweza kukamatwa kupitia
doria na misakombalimbali.
Ngonyani ameeleza kuwa kati ya
wahamiaji hao haramu 14 waliokamatwa 9 wananatoka nchi ya Burundi huku wa 4
wakiwa raia wa Ethiopia na 1 akiwa raia wa Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo.
Amesema kuwa wahamiaji hao
watafikishwa mahakamani baaada ya taratibu kukamilika ili kujibu tuhuma zinazo
wakabili za kuingia nchini bila kibali.
Amewaomba wananchi wa Mkoa wa
Katavi kutoa taarifa kwa jeshi hilo hususani zinazohusu wahamiaji haramu pamoja
na makosa mengine ili kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama kwa wananchi wa
Mkoa wa Katavi.
Katika taarifa hiyo ya Jeshi la
Polisi Mkoa wa Katavi imebainisha kuwa limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 84
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.
Watuhumiwa 22 wamekamatwa wakiwa
na dawa za kulevya aina ya bangi kete 136 huku watuhumiwa 12 wamekamatwa wakiwa
na Pombe haramu ya Moshi[gongo] lita 105.
Aidha Jeshi hilo la Polisi Mkoa
wa Katavi limefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 11 wakiwa na Pikipiki
zinazodhaniwa za wizi ambazo 7 kati ya hizo hazina namba za usajili.
Amefafanua kuwa Pikipiki 7 walizokamatwa
na watuhuhumiwa hao zinanamba za usajili wa MC.504 BVM aina ya Kinglion
Pikipiki nyingine ikiwa na namba za usajili MC.946 DSC aina ya Kinglion na MC
556 EKE aina ya Haojue.
Pikipiki nyingine iliyokutwa na
watuhumiwa hao ni MC.313 DVD aina ya Fekoni,MC 923 DGX aina ya Sanlg pamoja na
Pikipiki MC.511 EAZ aina ya Haojue na Pikipiki MC 639 AXA aina ya TVS.
Aidha Jeshi hilo la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 4 waliohusika katika matukio ya ubakaji kwenye maeneo tofautitofauti ya Mkoa wa Katavi.