Aliekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe Catheline Mashalla [aliekaa mbele]akiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda ambae kwa sasa ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa |
Na Paul Mathias-Katavi
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Katavi imewafikisha
Watuhumiwa 14 waliokuwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe Mkoa wa Katavi kwa
Makosa 153 ikiwemo kosa la uhujumu uchumi.
Watuhumiwa wengine wa Makosa ya uhujumu uchumi wakiwasili katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwaajili ya kusomewa Mashitaka hayo |
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Katavi imewafikisha Watuhumiwa 14 waliokuwa watumishi wa Halmashauri ya Mpibwe Mkoa wa Katavi kwa Makosa 153 ikiwemo kosa la uhujumu uchumi.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa Habari Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi Stuart Kiondo
amesema kuwa mwaka jana Takukuru ilifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu mkazi
mkoa wa Katavi kesi ya uhujumu uchumi namba 5 ya mwaka 2023 katika kesi hiyo
kulikuwa na watuhumiwa Nane.
Stuart Kiondo Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari kuhusu makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha yanayowakabili watuhumiwa hao |
Walioongezeka
katika Kesi hiyo ni Pamoja na Aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Mpibwe Mkoa wa Katavi Catheline Mashallah ambae kwa sasa ni Mkurugenzi wa
Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa Mwingine ni ,Mhamed Lungia,Flaviani
Mkombozi watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe.
Wengine
walioongezeka katika kesi hiyo ni Ntelugwa Ali Udu,Juma Motera Jonh Oluomba,
,Ahamed azizi Dugange ,Bhoke Thomas Ngorongoro,pamoja na kampuni ya uzalishaji
wa Mafuta ya Alizeti kinachopatikana Itigi Mkoa wa Singida kinachomilikiwa na
Tumaini Richard Msese.
Baadhi
ya Makosa wanayotuhumiwa nayo washitakiwa hao ni pamoja na Uhujumu Uchumi,Utakatishaji
wa fedha,Kuunda Genge la Uhalifu,na Kugushi Malipo kwa njia ya mtandao kinyume
na utaratibu.
Kelvini
Mwaja Mwendesha Mashitaka wa Serikali amesema kuwa pamoja na kuongeza
washitakiwa katika Shauli hilo jamhuri imeongeza baadhi ya Mashitaka na kufikia
Mashitaka 153.
Mwaja ameeleza kuwa washitakiwa wote wanashitakiwa kwa kuisabishia serikali hasara ya Shilingi Bilioni 1 na Milioni 232 ikiwa ni kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.
Katika utetezi wao watuhumiwa hao wameiomba Jamhuri kuharakisha upelelezi wa Kesi hiyo ili ianze kusikilizwa kwakuwa wamekaa lumande zaidi ya miezi Minane sasa.
kesi hiyo itatajwa tena 28/3/2024 Katika mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Katavi.