Na Walter Mguluchuma,Katavi
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi imewafikisha Mahakamani watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi akiwemo mtunza hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye akaunti za watu binafsi .
Watumishi wa Halmashauri ya Mpimbwe wakiwa wanaingia katika jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Katavi chini ya ulinzi wa Maofisa wa Takukuru |
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Katavi imewafikisha Mahakamani watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpibwe Mkoani Katavi akiwemo mtunza hazina wa Halmashauri hiyo kwa kutuma za wizi wa zaidi ya shilingi Bilioni 1.2 walizokuwa wakiziingiza kwenye akaunti za watu binafsi .
Mkuu
wa Takukuru Mkoa wa Katavi Faustine Maijo
amewataja watuhumiwa hao waliofikishwa
Kizimbani na Takukuru Mkoa wa
Katavi kuwa ni Canuthe Matsindiko,
Michael Katanga(Big),Masami Mashauri
ambae ni mweka hazina wa
Halmashauri hiyo(DT) Tumaini
Misese,Maila Oluomba ,
Emanuel Salanga na
Laurent Sunga.
Maijo alisema
watuhumiwa hao wamefikishwa
Mahakamani na kusomewa mashitaka
katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Katavi na kusomewa mashitaka na mbele ya
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
hiyo Gwai Sumai
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Katavi,Faustine Maijo akieleza mbele ya waandishi wa Habari juu ya kufikishwa Mahakamani kwa watuhumiwa saba wa Halmashauri ya Mpimbwe. |
Amebainisha kuwa
kabla ya kukamatwa kwa watumishi
hao Takukuru Mkoa wa Katavi walipokea
taarifa juu ya ubadilifu wa fedha katika
Halmashauri ya Mpimbwe ulikuwa ukihusu wizi wa fedha kiasi cha
Tshs 1,232 869,000 fedha hizo zikuwa kwenye
akaunti ya Halmashauri ya
Mpimbwe na walizifuja kwa kusingizia kuwa waliwalipa wakandarasi ambao walifanya shughuli mbalimbali jambo
ambalo halikuwa na ukweli .
Maijo alisema
uchunguzi waliofanya wamebaini
fedha hizo walizilipa kwa watu binafsi
ambao hawakuwa na kazi yoyote
walizofanya katika Halmashauri hiyo
lakini waliwalipa watu ambao walikuwa wakifahamiana nao kwa kibali kuwa wamewalipa wakandarasi
waliokuwa wakifanya kazi za ukandarasi mbalimbali .
Watumishi
hao wamefikishwa Mahakamani na kusomewa mashita matatu shitaka la kwanza wameshitakiwa kujihusisha na genge la
uhalifu shitaka la pili ni la uhujumu
uchumi na shitaka la tatu ni wizi
.
Washitakiwa hao kwa pamoja wameshitakiwa kwa makosa
ya uhujumu uchumi kinyume cha aya ya nne
[c ]na kifungu cha 57(1) 60 ( 2 )
cha sheria ya uhujumu uchumi sura
ya 200
marejeo ya 2022 washitakiwa
hao wote wanadaiwa kama watumishi wa
Halmashauri hiyo kwa pamoja waliunda
genge la uhalifu kwa lengo la kujipatia
manufaa walifanya matukio kwa mtililiko kwa lengo la kufanana na kujipatia manufaa ya kiasi hicho cha fedha
.
Shitaka
la pili wanashitakiwa washitakiwa kwa
kosa la kuisabishia Halmashauri hasara kinyume na kosa la kifungu
cha sheria sura ya 10(1) na 57 [1] na 60[2] sura ya 200 Marejeo ya 2022
Kosa
la taui ni wizi ambalo
wameshitakiwa kinyume na kifungu cha
sheria namba 265 na 270
kinyume na kifungu kanuni ya adhabu sura marejeo ya 2022 kwa pamoja wanadaiwa kuiba
kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 kwa kuwa
ni watumishi wamekiuka kifungo cha sheria namba 270 kwa kufanya wizi wakiwa
watumishi wa umma .
Watuhumiwa hao baada ya kusomewa mashita waliambiwa na
Mahakama kuwa hawatakiwi kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Katavi
haina mamlaka ya kusikiliza kesi
hiyo ya uhujumu uchumi mpaka mahakama ya juu zaidi ya hiyo .
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Katavi Gwai Sumai alihairisha kesi hiyo hadi hapo septemba 4 na watuhumiwa hao wote saba waliamriwa kwenda katika gereza la mahabusu la Mpanda mjini hadi hapo siku ya tarehe hiyo
Kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com