Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Mwl Alexius Kagunze
Na George Mwigulu,Katavi.
Afisa Mtedaji wa Kijiji cha Kaulolo,Kata ya Nsenkwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi,Jackson Shula amemkamata na kumweka mahabusi mama mkwe wake kwa kosa la ku tompeleka shule mwanae ambaye ni shemeji wa afsa mtendaji huyo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtedaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele,Mwl Alexius Kagunze alipoeleza kwenye kikao cha wadau wa elimu kilichohudhuriwa na Juma Homera,Mkuu wa Mkoa wa Katavi namna serikali imejipanga kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kuwa wanahudhulia.
Kagunze ameeleza hatua hiyo imechukuliwa na afisa mtendaji Jackson kwa Mama Mkwe wake ,Elizabeth John mkazi wa kijiji cha Kaulolo kutokana na kumficha porini mtoto wake wa kike (Jina limehifadhiwa) mwenye umri wa miaka 13 huku akimtumikisha kwenye mashamba kwa siri katika kitongoji kidogo cha Sangali wilayani humo.
Amebainisha kuwa hali ya uchumi wa mama huyo sio ya kutiliwa shaka kutokana na kuwa amejijenga kimaendeleo kwa kazi mbalimbali anzozifanya za kumwingizia kipato,Hivyo hakuwa na sababu ya kushindwa kumpeleka shule aliyochaguliwa binti yake kujiuga nayo kidato cha kwanza katika Sekondari ya Issack Kamwele.
''...lengo kuu la Elizabeth John lilikuwa ni kumficha binti yake kwa ajili ya kutaka kumwozesha ili aweze kunufaika kwa kujipatia mahali.Kitendo ambacho kama mimi mkurugenzi siwezi kukubaliana nacho hata kidogo na hatua kali lazima itachukuliwa dhidi yake" alisema Mkurugenzi huyo.
Katika hatua nyingine ameweka wazi kuwa kati ya wanafunzi 635 waliokuwa wanatakiwa kujiunga kidato cha kwanza katika halmashauri ya Mlele ni wanafunzi 14 hawajaripoti na katika wanafunzi 14,Wanafunzi 10 wamedhibitisha kuhama na wazazi wao kutokana na kuwa ni jamii ya wafungaji.
Mikakati hiyo imefanikiwa kwa asilimia 98 watoto kujiunga na kidato cha kwanza na kuwa ya kwanza katika Mkoa wa Katavi ikiwa pamoja na kutokuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa huku wakiwa na ziada ya madawati 150 katika shule ya sekondari Ilunde.
Afisa Mtedaji wa Kijiji cha Kaulolo,Kata ya Nsenkwa Jackson Shula alipozungumza na gazeti Majira kwa njia ya simu alisema kuwa kitendo alichokifanya cha kumweka mahabusu mama mkwe wake ni kwqa ajili ya kutete masirahi na haki ya mtoto wa Afrika ambaye kwa muda mrefu amekuwa wakikosa elimu.
'' ni kazi ngumu sana kumweka mama mkwe wako ndani ukizingatia ndiye aliyekuzalia mke wako wa ndoa,Lakini mefanya hivyo kwa moyo kupenda kwa ajili ya shemeji yangu ambaye anauwezo mkubwa darasani na alikuwa hatarini kukosa elimu"alisema Jackson.
Juma Homera,Mkuu wa Mkoa wa Katavi ametoa wito kwa maafsa elimu wote kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuwa wanaripoti bila kukosa kinyume na hapo hatua kali zitachukuliwa.
Amesema kuwa suala la uhaba wa madawati linapaswa kushughurikiwa kwa haraka zaidi kwani kama tatizo hilo halitashughurikiwa kutazorotesha ukuaji wa elimu wa mkoa.