|
Baadhi ya mifugo ya ng'ombe inayomilikiwa na akimama wa Mkoa wa Katavi. |
Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Taasisi
ya Kawodeo inayojishughulisha na maswala ya utunzaji wa mazingira na
msaada wa kisheria katika Mkoa wa Katavi imepanga kutowa elimu kwa
jamii ya akina mama wafugaji wa mifugo ili wajuwe haki yao
ili waweze kuondokana na changamoto hiyo .
Hayo
yalisemwa hapo jana na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya
Kawodeo Fujensiana Kapama wakati alipokuwa akiongea na wandishi wa
habari juu ya utendaji kazi unaofanywa na Taasisi hiyo.
Alieleza
kuwa kumekuwa na changamoto kwa akina mama wa jami iya
wafugaji walio wengi kutojua haki zao za msingi i za kibinadamu
kutokana na uwelewa mdogo wa kujua haki zao .
Hivyo
kwa kutambua hilo taasisi hiyoimepanga kuzunguka kwenye maeneo yote ya
Mkoa huu kwa lengo la kutowa elimu kwa akina mama wa jamii ya wafugaji ili
waweze kuelewa haki zao .
Bi
Kapama alisema kuwa watoto wengi ambao wamekuwa wakipewa mimba wakiwa na
umri mdogo ni watoto wa wafugaji na wamekuwa hawajui hata kama
watoto wao wamepewa mimba wapeleke wapi malalamiko yao ili hatua
zichukuliwe.
Alifafanua
kuwa wanawake wa kifugaji wamekuwa wakihamishwa na waume
zao kutoka maeneo ya Mikoa mingine kwenda kwenye mikoa
mingine kama wao ni mizigo na wala hata wao bila kutaka .
Wamekuwa
wanapelekwa hata kwenye maeneo ambayo hayana maji na wamekuwa
wakilazimika kutembea umbali wa kilometa nne kupata huduma ya maji
na yote hiyo imekuwa ikitokana na kutojua haki zao za msingi .
Alisema
kuwa wamekuwa wakifanya hamasa kwa wanawake na makundi
ys pembezoni katika kusimamia na kufanya maamuzi
juu ya rasirimali .
Nae
Maria Kaboza Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kitoleni Kata
ya Stalike Halmashauri ya Nsimbo alieleza kuwa siku za nyuma
wanawake walikuwa wakinyanyasika lakini hivi sasa wanamiliki mali
kutona na kazi ambayo imefanywa na taasisi hiyo kwa kutowa elimu kwa wanawake .
Alisema
kulikuwa na mila potofu ambazo zilikuwa azimtambui
mwanamke kuwa hawezi kumiliki mali kama vile ardhi
lakini kutoka na elimu sasa hivi wanapata kumiliki ardhi.