Meneja wa Chama kikuu cha ushirika Latcu Mkoa wa Katavi Pius Kilo akizungumnza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 32 uliofanyika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda
Na Mwandishi wetu-Katavi
Wakulima wa zao la Tumbaku katika Mkoa wa Katavi wameonywa kuacha tabia ya kuchanganya vitu visivyo faa kwenye zao la Tumbaku kwa lengo la kuongeza uzito wa zao hilo wakati wa Masoko.
Wakulima wa zao la Tumbaku katika Mkoa wa Katavi wameonywa kuacha tabia ya kuchanganya vitu visivyo faa kwenye zao la Tumbaku kwa lengo la kuongeza uzito wa zao hilo wakati wa MasokoAgizo hilo limetolewa na Meneja
wa Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Katavi LATCU Pius Kilo wakati wa mkutano
mkuu wa 32 mwaka uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Amesema kuna baadhi ya wakulima
wamekuwa wakichanganya Vitu visivyo faa kwenye zao la Tumbaku hali ambayo
imekuwa ikipelekea kutaka kuharibu soko la Tumbaku kwa wakulima wa Mkoa wa
Katavi na Tanzania kwa ujumla.
![]() |
| Froria Haule Mkurugenzi wa Maendeleo ya ushirika shirikisho la vyama vya ushirika Tanzania akitoa neno kwenye mkutano Mkuu wa 32 wa Chama kikuu cha Ushirika Latcu Mkoa wa Katavi |
Katika hatua nyingine amesema zao
la Tumbaku nimiongoni mwa mazao yanayoipatia nchi fedha za kigeni ambazo
husaidia ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya maendeleo kwa wanannchi huku
akisistiza wakulimakujiepusha kuchanganya ngulai kwenye Tumbaku zao wakati wa
Masoko.
Ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya Amcos kwenda kusimamia ubora wa zao hilo bila kufanya uchafuzi wa aina yeyote ile kwakuwa kufanya hivyo kunazidi kupunguza sifa kwa wanunuzi wa ndani na wanunuzi wanje.


