Balozi wa Utalii hapa nchini Nangasu Warema akiongea na wadau wa Utalii mkoa wa Katavi katika kongamano la utalii lililofanyika mkoa wa Katavi. |
Na Paul Mathias-Katavi
Wananchi katika mkoa wa Katavi wameobwa kujenga utamaduni wa Kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kama sehemu ya uzalendo na kukuza utalii wa ndani.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Onesmo Buswelu akimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Katavi katika kongamano hilo |
Wananchi katika mkoa wa Katavi wameobwa kujenga utamaduni wa Kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi kama sehemu ya uzalendo na kukuza utalii wa ndani.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi
wa Mkuu wa Mkoa wa Onesmo Buswelu wakati akiwa hutubia wadau wa Utalii katika
Kongamano la Kampeni ya Utalii na Mama Samia Hifadhi ya Taifa ya Katavi
lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Bwalo la Polisi Mpnda Mjini.
Wadau mbalimbali wa utalii wakiwa katika kongamano la utalii katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Mpanda Mjini |
‘’Tupende kuthamini vya kwetu na wengine watavipa thamani kubwa tukivichukia vya kwetu hayupo atakakae kuja kuvipenda vya kwetu tuipende mbuga yetu ya Katavi kwa kuitembelea na kwenda kujionea wanyama mbalimbali’’amesema Buswelu.
Ameeleza kuwa kutalii kunafaida ikiwemo kupunguza mawazo na kuongeza utimamu wa akili katika kukabiliana na Majukumu ya Kila siku .
’'Kutalii kunaongeza utimamu wa akili unakuwa na Maisha Mapya kwa wakati huo twende tukatalii tuwahimize watu tuhamasishe waje kutalii”amesisitiza BusweluKwa upande wake Balozi wa Utalii Tanzania
aliyekuwa Mgeni Mwalikwa katika
Kongamano hilo Nangasu Warema amesema kuwa kupitia utalii kunaongeza vipato vya
uchumi kwa wananachi wa mkoa wa Katavi na kuawasa wananachi kutembelea hifadhi
ya Taifa Katavi.
‘’Watalii watakapokuja Mpanda
watawekeza Mama Ntilie atapata hela,Nyumba za kulala Wageni zitapata hela
lakini pia kule hifadhini Mapato yataongezeka na taifa litaingiza Pesa amesema
Warema’’
Amesema kama Balozi wa Utalii hapa nchini
amekuwa akitembea mikoa mbalimbali hapanchini kwa lengo la kuhamasisha utalii
na kwa lengo la kuhakikisha wananachi na wadau wa utalii hapa nchini wanakuwa
mabalozi wazuri kuhusu utalii kwa kutenbelea vivutio vya utalii.
Thomas Ngozi mmoja wa Washiriki
katika Kongamano hilo amesema wakati umefika sasa kwa serikali ya Mkoa wa Katavi
kupitia mamlaka zinazo husika kuendeleza maeneo mbalimbali ya uhifadhi na mali
kale zilizopo mkoa wa Katavi ili kizazi Kijacho kiwe sehemu ya wanufaika na
utalii.
‘’Mkoa huu unavivutio vingi vya
utalii mfano kuna mlima wa Lyambalya Mfipa maeneo haya yakitunzwa na kutangazwa
yatakuwa na tija katika vizazi vijavyo anasema Thomas Ngozi’’
Kwa upande wake Teddy Kapufi
mmoja ya washiriki wa Kongamano hilo ameomba gharama za kuingia katika hifadhi
ya Taifa ya Katavi ikiwa ni sehemu ya kuvutia makundi yenye kipato cha chini
kutembelea hifadhi hiyo hususani wakazi wa mkoa wa Katavi.