![]() |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani |
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Busu Lugwisha(51) mkazi wa Kijiji cha Masigo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumuua mke wake aitwaye Regina Thobias (40) kwa kumpiga na kitu kizito chenye mcha kali kichwani baada ya kunyimwa tendo la ndoa na mkewe kwa muda mrefu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Busu Lugwisha(51) mkazi wa Kijiji cha Masigo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumuua mke wake aitwaye Regina Thobias (40) kwa kumpiga na kitu kizito chenye mcha kali kichwani baada ya kunyimwa tendo la ndoa na mkewe kwa muda mrefu.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster
Ngonyani amesema tukio hilo la mauaji hayo ya
kusikikisha limetokea Februari 19 majira ya saa kumi usiku
nyumbani kwa wanandoa hao wawili waliokuwa wakiishi wakiwa mume na mke .
Kamanda Ngonyani amesema chanzo
cha mauaji hayo ya mwanamke huyo kilitokana na wivu wa
mapenzi kwa kile kunachodaiwa ni hasira zamthumiwabaada yakunyimwa
tendola ndoa na Ragina Thobias ambae alikuwa ni mke wake .
Amefafanua kuwa kutokana na wivu huo
wapenzi ndio ulimfanya mtuhumiwa Busu kumpiga kichwani
na kitu kizito kichwani upande wa kisogoni na
kumsababishia mkewe kufa hapo hapo .
Ameeleza kuwa katika mahojiano ya awali na mtuhumiwa
jeshi la polisi limebaini mauaji hayo yametokana na
wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kukiri kufanya mauaji hayo kwa kile
alichodai kuwa mkewe alikuwa amenyima tendo la ndoa kwa muda mrefu sasa .
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba
cha kuhifadhi maiti katika kituo cha afya cha Inyonga B kwa ajiri ya
uchunguzi zaidi na mara uchunguzi utakapokuwa umekamilika watakabidhiwa ndugu
wa marehemu kwa ajiri ya mazishi .
Kamanda Ngonyani amesema mtuhumiwa
bado anaendelea kushikiliwa na polisi na mara upelelezi ukikamilika
atafikishwa mara moja mahakamani ili akajibu tuhuma zinazo mkabili .
Jeshi la Polisi linatowa wito watu waache tabia ya kujichukulia sheria mikononi na badala yake wawasilishe changamoto zinazowakabili kwa viongozi wao wa familia dini mitaa au mamlaka za kisheria kwa ajiri ya utatuzi .

