WATAADHARISHWA MAGONJWA YA MLIPUKO KUSABABISHA ULEMAVU WA KUDUMU.


 Na George Mwigulu KTPC,Mpanda.

Wananchi wa Halmashuri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi wameombwa kutambua mapema athari zinazoweza kusababishwa na magonjwa ya mlipuko ya Polio na Surua kuwa yanaweza kusababisha ulemavu wa kudumu kwa wangonjwa kama hawatapatiwa matibabu haraka.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko wa Hosptali teule ya rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Taphinez Machibya wakati alipokuwa akizungumza na Katavi Press Club Blog ofisini kwake.

Dkt Machibya ameweka wazi kuwa magonjwa ya mlipuko ya Polio na Surua ni hatari sana kwenye ustawi wa mtu,kwani magonjwa hayo yanaweza kumfanya mwathirika kuwa mlemavu wa kuduma kama hatua hazitachukuliwa.

Anaeleza kuwa Ugonjwa surua na polio yanaweza kuua au kusababisha madhara ya muda mrefu lakini  chanjo dhidi yake inazuia hatari hiyo.Kwahiyo pale unapohisi mtoto anakuwa na dalili za surua na polio ni vema apelekwe haraka hospitali ili kujithibitisha na kupata matibabu yanatofaa.

Amesema kuwa katika athari ambazo mgonjwa zinazoweza kumsababishia ulemavu wa kudumu ni kutokana na virusi hivyo inahusishwa na aina mbalimbali ya mashambulizi kwenye ubongo kama vile kitaalamu acute encephalitis ambayo hutokea wakati au ndani ya wiki chache baada ya maambukizi ambapo mtoto anaweza kupelekewa kuwa na mtindio wa ubongo na kupuguza uwezo wake wa akili kuchakata mambo kwa haraka na kuyashika pia.

Surua kwa sababu hupunguza Vitamin A na kusababisha tatizo la kutoona vizuri ambalo hujulikana  kama Keratitis,Kwa watoto wadogo ambao wanaupungufu wa vitamin A tatizo la macho huwa kubwa zaidi  na kwa kitaalamu hujulikana kama Keratomalacia ambapo sehemu ya jicho hutoboka.

“ wananchi wanapaswa kutambua umuhimu wa chanjo mapema ya magonjwa haya…ni hatari kwa sababu yanaweza kusababisha upofu kwa mtu.Na kama unavyofahamu ndugu mwandishi tumeona kwa macho au kwa kusimuliwa kuwa kunawapendwa wetu wengi tumewashuhudia wakipatwa na upofu kwa sababu ya ugonjwa wa surua”alionge kwa kusisitiza Dkt Machibya.

Ulemavu mwingine unaowezwa kusababishwa na ugonjwa wa mlipuko wa surua ni ulemavu wa ngozi.

Katika ugonjwa wa mlipuko wa polio Dkt Machibya amesema kuwa ugonjwa huo kutokana na kuathri zaidi mifupa  ya mtoto pamoja na kumfanya kudumaa kwa kushindwa kukua vizuri,Hivyo hupelekea kupata ulemavu wa viungo.

Aidha surua na polio huzuiwa kwa njia rahisi sana kwa njia ya chanjo,Watoto ambao hawajapata chanjo ya surua,polio  wapo katika hatari kubwa sana kupata magonjwa hayo,Hivyo aliitaka jamii kutambua madhara yanayosababishwa na magonjwa ya mlipuko kuwa yanaweza kumsababishia mtu ulemavu mkubwa hivyo suala la kuchukua hatua za chanjo ni muhimu.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Dotto Hussein alikili kuwa baadhi ya wanajamii amewashuhudia kupata ulemavu uliosababishwa na magonjwa ya mlipuko kitendo ambacho hapo awali walikuwa wakihusisha na imani za kishirikina.

Dotto anaeleza kuwa jamii haikuwa tayari kukubaliana na hali za ulemavu wa watoto wao kuwa umesababishwa na magonjwa ya mlipuko hivyo kupelekea visasi vya kuuwana.Lakini baada ya kutolewa kwa elimu jamii imekuwa na uelewa mkubwa wa namna ya kujikinga na magonjwa hayo.

Mwanaidi Omary anasema kuwa baadhi ya watoto kuathirika na magonjwa ya mlipuko na kupatwa na ulemavu wa utindio wa ubongo au ulemavu wa viongo jamii ilikuwa inawatenga watoto hao kwa imani kuwa wamelengwa au ni laana ndani ya familia,Hivyo kupelekea kushindwa jamii kutafuta suruhisho la magonjwa hayo ya mlipuko na kupatiwa chanjo.

Aidha anaongeza kuwa kutokana na juhudi ambazo zimefanywa na serikali kupitia wizata ya afya jamii sasa imeelimika na kuhakikisha wanafika katika vituo vya kutolea afya kwa ajili ya chanjo ambapo visa vya watoto walemavu vimepungua kwa kasi.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages