Mkurugenzi wa Taasisi ya Usevya Development Eden Wayimba akifungua mafunzo kwa wajumbe wa kamati za Pets kutoka vijiji vya Lugonesi na Kasekese. |
Katavi
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Usevya Development Sociaety(UDESO) imeanza kutekeleza mradi wa Audit Accountability Initiative(AAI) katika Wilya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ukiwa na lengo la kuangalia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika Sekta ya Elimu ya msingi na awali kupitia ripoti iliyotolewa na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Usevya Development Sociaety(UDESO) imeanza kutekeleza mradi wa Audit Accountability Initiative(AAI) katika Wilya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ukiwa na lengo la kuangalia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika Sekta ya Elimu ya msingi na awali kupitia ripoti iliyotolewa na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
Hayoyamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Usevya Development Society Eden Wanyimba wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za PETS wa kutoka katika Vijiji viwili vya lugonesi na Kasekese yatakayo wawezesha kufanya majukumu yao kwa ufasaha watakayopangiwa katika muendelezo wa utekelezaji wa wa radi huu[ AAI]
Mafunzo
hayo yatawawezesha kubaini vikwazo
mbalimbali vinavyiikumba miradi
ya maendeleo katika Vijiji vyao
na kushauri namna bora ya
kufanya ili kuifanya miradi ya maendeleo
katika jamii zao kwa ufanisi wa hali ya juu.
Amefafanua
kuwa Mwezi March Mwaka huu walitambulisha Mradi kwa ngazi tofauti tofauti
kuanzia ngazi za Vijiji ambavyo Mradi huu unatekelezwa baada ya utambulisho huo
kamati za Pets kutoka katika vijiji hivyo viliundwa kupitia serikali zao za
mitaa na wanavijiji wa Vijiji vya Lugonesi na Kasekese zikiwa na wajumbe 10
wanawake Watano na wanaume Watano.
Amesema
mbali ya Mradi huu UDESO imekuwa ikiwezesha Maendeleo ya Jamii Katika sekta
Mbalimbali kwa kushirikiana na wadau tofautitofauti miongoni mwa sekta ambazo
UDESO wameshirikiana nazo nipamoja na Sekta ya Afya,Elimu,Mazingira,Maendeleo
ya Jamii Jinsia wazee na watoto,Kilimo,na Technolojia ya habari na Mawasiliano.
Washiriki wa Mafunzo ya kamati za Pets wakiwa katika Semina hiyo. |
Elizia
Feston Mjumbe wa Pests kutoka kijiji cha Kasekese amesema mafunzo hayo
aliyoyapata yatamsaidia kusimamia miradi ya maendeleo katika kijiji hicho
itakayojitokeza japo kwa sasa miradi iliyopo niyamajengo ya Sekta ya Elimu.
Amesema
baada ya Mafunzo haya atakwenda kuwaelimisha wananchi kijijini kuweza
kusimamamia miradi yote pasitokee ubadilifu kwenye miradi itakayo letwa na
serikali kwakuwa Mradi huo ameupokea vizuri bila mashaka yeyote baada ya
kupatiwa mafunzo hayo atafanya kazi vizuri.
Amesema washiriki hawa wameelekezwa kushiriki katika kuyapunguza au kuziondoa kabisa Maazimio ambayo yaliibuliwa na CAG kwenye Ripoti yam waka 2017 kwenye Elimu.