CCM TANGANYIKA YAKERWA NA MAFUNDI UJEZI KUTOLIPWA FEDHA ZAO.

 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi,Yasini Kiberiti (mbele) akikagua ujenzi kituo cha Afya Kasekese wilayani humo
Na Mwandishi Wetu KTPC,Tanganyika.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Yasini Kiberiti ameitaka halmashauri ya wilaya hiyo kuhakikisha inamlipa kwa wakati malipo ya awali ya fedha ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kasekese.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ukaguzi wa miradi mitatu katika Kata ya Kasekese aliyoifanya jana kwenye sherehe ya maadhimisho ya miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo alitembelea ujenzi wa kituo hicho cha afya,Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari ya Kata hiyo pamoja na ukaguzi wa stand ya mabus.

Kiberiti alisisitiza kuwa Fundi Ujenzi,Michael Kalinde  ambaye ni mjezi wa Kituo cha Afya Kasekese amecheleweshewa malipo yake kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika kwani licha ya serikali kutoa fedha za malipo hayo lakini ameshindwa kulipa.

Alieleza kuwa suala kuwacheleweshea mafundi ujenzi wa miradi mbalimbali linaathari kubwa kwa miradi husika kwani ni chanzo kikubwa kwa miradi ya umma kujengwa chini ya kiwango huku na kutokea ubadhirifu wa kuhujumu vifaa vya ujenzi kwa kuimba.


Mhadisi wa Halmashauri ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Eng,Salun Ibrahimu(wa kwanza kushoto) akiwaeleza kamati ya siasa ya wilaya hiyo ya chama cha mapinduzi walipotembelea kituo cha afya Kasekese.


Aidha alisema kuwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Tanganyika katika kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo wamebaini kuwepo kwa baadhi ya serikali za vijiji kuwa na akauti za benk zilizokufa na kushindwa kupokea fedha za miradi ya maendeleo.

Alibainisha kuwa kitendo hicho ni ishara tosha ya kuwa viongozi wa serikali hizo hawatoshi kwenye nafasi hizo za uongozi kwani ni wazi fedha ambazo wanazipokea za miradi mbalimbali wanazifanyia ubadhirifu,Hivyo amewataka wenyeviti wa vijiji pamoja na maafisa watendaji kijiji na kata kushughurikia kwa wakati uhuishaji wa akauti za benki zote zenye matatizo hayo.

Mhadisi wa wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi,Salum Ibrahim alisema kuwa mradi wa jenzi wa kituo cha afya Kasekese hadi kumalika utagharimu jumla ya fedha milioni 167 ambapo kwa sasa umetumija fedha Milioni 70.

Salum akifafanua kucheleweshewa malipo ya fedha kwa fundi ujenzi ni kutokana na fedha za mradi huo kuinginzwa kwenye akauti ya benki ya kijiji kingine kwani kijiji cha Kasekese kutokuwa hai hivyo ili fedha hiyo iweze kutoka ni lazima taratibu zingine zifanyike.

Mwonekano ya shule ya sekondari Kasekese Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi


Kwa upande wa kaimu Katibu wa CCM wilaya ya Tanganyika,Adelaida Paschal alisema kuwa chama kiko makini kaiika kufuatlia miradi ya serikali na haitakubali hujuma yoyote ifanya ili kukwamisha.

Adelaida alifafanua kuwa suala la uadulifu ni muhimu katika utekelezaji wa miradi maendeleo kwani itakuwa chachu ya kuikamilisha kwa wakati sahihi huku ikiwana na ubora unaotakiwa kwa viwango vya serikali.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages