WAZAZI/WALEZI MLELE WATAKIWA KUPELEKA WATOTO SHULE



Na Mwandishi Wetu KTPC,Mlele

Wazizi na Walezi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule ifikapo March 30.2021 kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa zidi yao kwa kushindwa kuwafikisha wanafunzi shule.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya   Mlele Mwl Alexus Kagunze amesema kuwa mzazi atakayeshindwa kumfikisha mwanafunzi shule hatua za kisheria zitachukuliwa zidi yake kutokana na serikali kwa sasa kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kupata Elimu.

Aidha katika hatua nyingine Kagunze ameeleza kuwa halmashauri hiyo haijawa na uhaba wa madarasa pamoja madawati na amewataka walimu kuto wafukuza wanafunzi kwa kisingizio cha sare za shule ili kuondoa wimbi la wanafunzi kuchelewa kuanza Masomo.

Katika hatua nyingi katibu Tawala wa Halmashauri ya Mlele Lincolini Tamba ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kusimamia zoezi la Kuripoti kwa Wanafunzi ambapo zaidi ya asilimia 80 wamefika shuleni huku akiwasisitiza Madiwani kwenda kwenye kata zao kuwahimiza wazazi kuwapeleka watoto wao shule.

Halmashauri ya Wilaya ya Mlele nimiongoni mwa Halmashauri zilizopo ndani ya Mkoa wa Katavi ambazo zimekuwa zikifanya vizuri katika mitihani.

 
 
 

 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages