Na Walter Mguluchuma KTPC, Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata Mganga wa Kienyeji mmoja aitwaye Mayala Hinyali mwenye umri wa miaka 34 Mkazi wa Kijiji cha Kasekese Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya kumtorosha S huleni mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 16 jina limehifadhiwa na kuishi nae kama mke wake .
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanikiwa kumkamata Mganga wa Kienyeji mmoja aitwaye Mayala Hinyali mwenye umri wa miaka 34 Mkazi wa Kijiji cha Kasekese Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi baada ya kumtorosha S huleni mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 16 jina limehifadhiwa na kuishi nae kama mke wake .
Mwanafunzi huyo alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi waliojiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwaka huu katika shule ya Sekondari Usevya Tarafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele .
Kamanda Kuzaga alieleza kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kumtorosha mwanafunzi huyo alimtowa kwenye Shule hiyo na kumsafirisha hadi kwenye Kijiji cha Kasekese ambako alikuwa akiishi na kuanza kuishi nae kama kama mke wake bila kujari kuwa msichana huyo nado ni mwanafunzi na haja fikia umri wa kuolewa .
Alisema jeshi la Polisi lilipata taarifa za Mganga huyo wa kienyeji juu ya kumtorosha mwanafunzi huyo kutoka kwenye shule aliyokuwa ameanza kusoma na kwenda kuishi nae akiwa mke wake .
Kufutia taarifa hiyo jeshi hilo lilianza kufanya msako kwa kushirikiana na uongozi wa Kijiji cha Kasekese wa kumsaka mtuhumiwa huyo Mayala Hinyali na ndipo walipo weza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa nyumbani kwake akiwa akiishi na mwanafunzi huyo mwenye umri mdogo wa kidato cha kwanza .
Kamanda Kuzaga alisema kuwa mtuhumiwa huyo bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ili aweze kufikishwa Mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi ili iwe fundisho na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo ya kukatisha ndoto za wanafunzi wa kike kumaliza masomo yao kwani kwenye Mkoa wa Katavi matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.
Katika hatua nyingine jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limefanya msako mkali wa kuwasaka wezi wa pikipiki kufatia wimbi kubwa lililokuwa limeenea katika Mkoa wa Katavi na katika msako huo wamefanikiwa kukamata jumla ya pikipiki kumi na mbili ambazo zilikuwa zimeibiwa na watuhumiwa kumi na tano wamekamatwa kwenye msako huo na wanashikiliwa na jeshi la Polisi .
Kamanda Benjamin Kuzaga aliwaambia Wandishi wa Habari kuwa watuhumiwa hao walikamatwa hapo machi tatu katika maeneo tofauti tofauti baada ya jeshi la Polisi kuwa limegundua mtandao wa watu wanaojihusisha na wizi wa pikipiki .
Alisema kuwa wahalifu hao baada ya kuwa wamefanikiwa kuiba pikipiki wamekuwa wakifuta chesesi namba pamoja na namba za injini ili zisiwe rahisi kugundulika kwa wenye umiliki wa pikipiki wanazokuwa wameziiba
Vielelezo hivyo vya pikipiki vipo katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda na watuhumiwa wote bado wanaendelea kushikiliwa na polisi na mara upelezi utakapo kamilika watafikishwa Mahakamani ili wakajibu tuhuma zinazo wakabili .
Kamanda Kuzaga ametowa wito kwa wananchi kufika kwenye kituo cha Polisi cha Mpanda Mjini ili waweze kuzitambua pikipiki zao zilizo ibiwa na wafike wakiwa na nyaraka halali ambazo zinazowathibisha kuwa wao ndio wamiliki halali wa mali hizo