Meya wa Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi,Haidary Summury akiendesha hivi karibuni kikao cha baraza la madiwani.
Na WalterMguluchuma KTPC,Katavi .Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetumia zaidi ya shilingi milioni 600 zilizotokana na makusanyo yao ya mapato ya ndani kwa ajiri ya kusaidia shughuli za miradi ya maendeleo .

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetumia zaidi ya shilingi milioni 600 zilizotokana na makusanyo yao ya mapato ya ndani kwa ajiri ya kusaidia shughuli za miradi ya maendeleo .
Hayo yamesemwa hapo jana na Mkuu wa Idara ya fedha wa Manispaa ya Mpanda George Mashauri wakati wa kikao cha robo ya tatu ya mwaka ya Baraza laMadiwani la Manispaa hiyo .
Amesema hadi kufikia mwezi Aprili Manispaa ya Mpanda wameisha kusanya asilimia 96 ya mapato yao ya ndani katika mwaka wa fedha wa 2020/2921.
Mkuu huyo wa idara ya fedha amebainisha kuwa kati ya fedha hizo walizokusanya za mapato ya ndani zaidi ya shilingi milioni 600 zimetumika katika kufanya miradi mbalimbali yamaendeleo .
Meya waManispaa ya Mpanda Haidari Sumury alisema kuwa Manispaa ya Mpanda wamejipanga kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo iliyopangwa inatekelezwa na inamalizika kwa wakati .
Amesema kuwa wanamatarajia makubwa sana ya kukusanya mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 100 kutokana na kuwa hadi sasa wamebakiza asimia nne kufikisha asilimia mia moja na kipindi hiki ni cha mavuno ya mazao.
Amewahimiza Madiwani kuhakikisha wanasaidia kusimamia kukusanya mapato kwa pidii kwenye maeneo yao ili Halmashauri izidi kupata mapato na mapato yao yasipotee.
Meya huyo wa Manispaa ya Mpanda alisema kuwa Halmashauri hiyo wameweka mikakati mizuri ya kukusanya mapato ili Halmashauri izidi kukusanya mapato.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amewataka Madiwani kuhakikisha fedha zilizotolewa kwenye maeneo yao zinafanya kazi miradi kama ambavyo zilivyokusudiwa na miradi hiyo iwe imekamilika hadi ifikapo june 30 mwaka huu vinginevyo fedha za miradi hiyo zitarudishwa Hazina.
Amesema kuwa hategemea kuona fedha za miradi zikirudishwa hazina hivyo madiwani wasimamie kwa karibu miradi hiyo kwa manufaa ya wananchi .
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Jamira Yusuph amesema kuwa kazi ya kukusanya mapato ni ngumu na inachangamoto zake hivyo inahitaji ushirikiano.
Dc huyo alijibu pia malalamiko yaliyotolewa na Baraza hilo la Madiwani juu ya malalamiko ya wafanya biashara wanaosafirisha mazao yao kwenda nje ya Manispaa hiyo ambao licha ya kuwa na leseni wamekuwa wakisumbuliwa na kutozwa tena ushuru kwenye Halmashauri nyingine za ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa.
Ambapo alisema kuwa utaratibu umeisha andaliwa wa kufanya kikao cha ujirani mwema ambacho kitawashirikisha viongozi wa Mikoa ya Katavi , Rukwa, Kigoma na Tabora .