Na Wandishi wetu Katavi
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamelalamikia kuwepo kwa ongezeko kubwa la watoto wanao zurula mitaani muda wa masomo huku wakipita kwenye nyumba za watu na kubeba vyuma vya aina mbalimbali pamoja masafulia ,ndoo za plasitiki na kwenda kuuza kwenye maaneo yanayonunua vyuma chakavu .
Humud Juma Mkazi wa Mtaa wa Majengo Manispaa ya Mpanda amesema changamoto hiyo imekuwa ni kubwa sana kwa watoto wanao pita mitaani tena wakati wa masomo na kufafuta vyuma chakavu ndoo za plasitiki na safulia ,
Samome John amebainisha kuwa imekuwa shida sana kwa watu wenye nyumba ambazo hazina uzio kwani ukiacha nje kidogo tuu vyombo vyako vya bati au ndoo zaaina zote unakuta wamebaba .
Ameomba mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kuondoo tatizo hilo la watoto wangepiga hata marufuku kwa wanao nunua vyuma chakavu na vitu vya plastiki kutofanya biashara ya na watoto na endapo hali hii itaendelea upo uwezekana wa kuzalisha watoto wakao kuwa wahalifu.
