Na Paul Mathias
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Jiuxing
Tanzania Mining Company Limited inayofanya kazi zake katika Vijiji vya Ibindi
na Mtakuja Hlmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi imesema kuwa Tangu waanze kazi
mwezi novemba Mwka jana 2022 wamesaidia jamiii katika Nyanja za
Elimu,Usalama,na Miundombinu.
Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Jiuxing Tanzania Mining Company Limited inayofanya kazi zake katika Vijiji vya Ibindi na Mtakuja Hlmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi imesema kuwa Tangu waanze kazi mwezi novemba Mwka jana 2022 wamesaidia jamiii katika Nyanja za Elimu,Usalama,na Miundombinu
Hayo yamebainishwa na Afisa uhusiano wa Mgodi huo Anselm Mjinga wakati akitoa taarifa ya utendaji wa Mgodi kwa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko alipotembelea Mgodi huo ili kujionea namana unavyofanya kazi zake.
Anselm amesema kuwa wamewkuwa lafiki na jamii
inayo wazaunguka kwa kuendelea kuwa na mahusaiano mema na jamii kwa kuweza
kusaidia jamii katika Nyanja za elimu na ulinzi kwa kusaidia ujenzi wa Kituo
cha Polisi katika kijiji cha Ibindi na hapa anasema
“hatuja fikia kwenye uzalishaji lakini kuna
mafanikio mfano kwenye ujirani mwema hii Kampuni ipo vizuri sana na viongozi wa
serikali kwa ujumla kwa kusapoti ujenzi wa kituo cha polisi Ibindi kwa kutoa
Tofali 40000 za Block zenye thamani ya shilingi Milioni 5 hivyo mkuu wa mkoa
tuna mahusiano mazuri na jamii amsema ‘’Anselm
Pamoja na hayo amebainisha kuwa katika sekta
ya elimu wamekuwa wakisaidia katika suala zima la Mdawati kwa shule
zinazopatikana katika Kwenye maeneo wanayofanyia kazi kwa lengo la kutambua
umuhimu wa elimu katika jamii hizo na Taifa kwa Ujumla.
“tumesapoti Madawati kwa shule ya Sekondari
Ibindi na Sekondari ya Kapalala kama ujirani Mwema tumetoa Madawati 60, Ibindi tumepeleka
madawati 30 na Kapalala tumepeleka Madawati 30”
Kuhusu ajira kwa vijana katika Mgodi huo
amesema hadi sasa wameweza Kuajiri watu 20
ambao wapo kwenye Mkataba na wanatalajia kuajili wafanya kazi 500 huku
kipaombele kikiwa kuajiri vijana kutoka vijiji vinavyozungukwa na Mgodi huo
pamoja na vijana kutoka halmashauri ya Nsimbo kwa kusaidia jamii kwenye suala
la Ajira.
Katika hatua anyingine amsema kuwa
kunachangamoto katika Mgodi wa Mtakuja ambapo kuna maeneo ya Ekari Mbili ambazo
wamiliki wake wanadai fidia ya kulipwa hivyo kuwapachangamoto katika kufanya
shughuli hiyo.
,,tunachangamoto moja kwenye Mgodi wa Mtakuja
kuna Ekari mbili za wamiliki wawili wale watu tulitamani tumekaa nao mezani
angalau waweze kutuachia hayo maeneo hata kwa kuwalipa fidia au kuwabadilishia
maeneo mengine ili tuweze kuendelea na shughuli za uzalishaji pale kuna mitambo
tayari imefika pale tulitamani tuweze kuijenga pale tunaobwa fidia ya hadi
Milioni 600 hii inatupa changamoto Mh Mkuu wa Mkoa tungeobwa kuasaidiwa katika
hilo ili tuendelee na kazi amesema Anselm.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko
amewakalibisha kampuni hiyo katika mkoa wa Katavi na kuchangamkia fursa ya
uwekezaji katika sekta ya madini kwa kutambua umuhimu wa wawekezaji.
![]() |
Mkuu wa mkoa wa Katavi,Mwanamvua Mrindoko wa kwanza [kushoto] akiwa katika mgodi wa Jiuxing Tanzania Companya Limited alipotembelea Mgodi huo |
Kuhusu changamoto ya Mgogoro baina ya wamiliki
wa ekari Mbili katika kijiji cha Mtakuja mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amemwelekeza
mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nsimbo kuona namna ya kulitatua kwakuwa
kawakuwa tayari limeshalipotiwa kwake.
“Kuhusu lile la mgogoro nimtake mkurugenzi
ambae alililipokea amabae lipo kwake alimalize kwa taratibu zilizopo na kama
itaonekana kwamba kuna matatizo zaidi mkuu wa wilaya pia yupo na mawakilishi
wake yupo hapa naamini kuptia ofisi hizi mbili kwa kushirikiana na meneja wa
madini Mkoa naamini tatizo hilo litakwisha vizuri”
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa serikali katika mkoa wa Katavi inaendelea kuwakalibisha wawekezaji kwa lengo la kusisimua uchumi wa mkoa wa Katavi kwa ujumla.