Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Zaidi y a Kaya 100O katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanaolima mazao yao kwenye eneo la Kampuni wamemwomba amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Samia Suluhu Hassan kuweza kutatua kutatua mgogoro wao wa ardhi na jeshi la wananchi ulidumu kwa kipindi cha muda mrefu sasa pasipokupatiwa ufumbuzi.
Zaidi y a Kaya 100O katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wanaolima mazao yao kwenye eneo la Kampuni wamemwomba amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Samia Suluhu Hassan kuweza kutatua kutatua mgogoro wao wa ardhi na jeshi la wananchi ulidumu kwa kipindi cha muda mrefu sasa pasipokupatiwa ufumbuzi.
Maombi hayo ya wananchi hao yametolewa hapo leo na wananchi hao waliokuwa wamekusanyika katika ofisi ya CCM Mkoa wa Katavi kwa lengo la kufikisha kilio chao .
Thomas Jeremia mmoja wa wananchi hao ambae ndie wahanga wa eneo hilo maarufu kwa jina la Kampuni alisema kuna jumla ya Kaya 1,100 ambazo zimeathiri katika mgogoro huo wa ardhi .
Amesema kuwa kuna watu tisa waliwahi kuvunjwa miguu na kulazwa hospitalini mwaka jana baada ya kupokea kipigo na wengine wamekuwa wakichomewa nyumba zao.
Hivyo wanamuomba Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania aweze kuwasaidia kutatua mgogoro huu ili wananchi waweze kupatiwa haki yao .
Amebainisha kuwa eneo hilo lina ukubwa wa ekari zaidi ya ekari 2000.
Zeno Kamsonki alisema kuwa mbaya zaidi wananchi hao ambao hapo walikuwa wanamiliki maeneo hayo wala hawaja wahi kulipwa fidia yoyote endapo kama jeshi la wananchi kama wangekuwa wanahitaji kumiliki eneo hilo kama ambavyo sheria zinazoelekeza .
Brijita Pascal alisema kuwa yeye ni mjane na alikuwa amelima mahindi mwaka huu na wanajeshi la wananchi walifyeka mahindi yake zaidi ya ekari mbili hari ambayo itamfanya mwaka huu ataishi kwa shida .
Ameeleza kuwa Askari hao pia wamekuwa na tabia ya kuwapiga wananchi na hata yeye mtoto wake mmoja alipigwa na kuvunjwa mguu.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Katavi Beda Katani aliwaeleza wananchi kuwa chama kimesikia malalamiko hayo .
Amesema wao kama chama swala hilo wameisha lipokea muda mrefu na wanasubiri maamuzi ya kutoka ngazi za juu juu ya mgogoro huo.