WAZIRI JAFO-KAMPENI YA MAZINGIRA KUZINDULIWA.

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo

 
Na Mwandishi Wetu KTPC,Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amesema Ofisi yake inaandaa Kampeni ya Mazingira itakayoenda sambambana na mashindano yatakayo husisha upandaji wa miti,utunzaji na usafi wa mazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amesema Ofisi yake inaandaa Kampeni ya Mazingira itakayoenda sambambana na mashindano yatakayo husisha upandaji wa miti,utunzaji na usafi wa mazingira.

Amesema hayo  kwenye kikao kazi na Menejimenti ya Ofisi yake kilichohudhuriwa na  waadishi wa habari  kilichofanyika katika Mji wa Serikali Mtumba,jijini Dodoma, Jafo amesema kampeni hiyo kubwa na ya aina yake itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania, Dk. Philip Mpango.

Uzinduzi huo utafanywa katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira duniani Juni 5, mwaka huu kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa kielelezo katika utunzaji wamazingira.

“Kampeni hii kubwa itahusisha Mikoa yote 26 na itahusu usafi na Utunzaji wa Mazingirakwa ujumla wake ambapo tuzo na zawadi zitatolewa kwa washindi katika ngazimbalimbali mara baada ya tathmini kufanyika na zawadi zitatolewa wakati wa Siku ya Mazingira duniani Juni 5, mwaka 2021,” amesema Jafo.

Kampeni hiyo pia itashindanisha Majiji, Manispaa, Halmashauri za Miji na Majiji, Kata naVijiji. Katika nyanja za elimu na Afya, Vyuo, Shule za Sekondari, Shule za MsingiHospitali, Zahanati na Vituo vya afya pia zitashindanishwa.

“Tunafahamu changamoto kubwa za usafiri katika mashule yetu na taasisi za elimu yajuu, zawadi kama Magari, Pikipiki, Vifaa vya kufundishia na kompyuta zitatolewa, piavifaa tiba katika sekta ya afya ikiwemo vitanda katika hospitali zitakazoibuka vinarazitatolewa,” Jafo amesisitiza.

Makundi mengine yatakayoshindanishwa ni pamoja na Viwanda, Migodi, Hifadhi zaTaifa, Madampo, Viwanja vya Ndege, Stendi za Mabasi, Masoko, Hoteli za nyota (1-5)na Waandishi wa Habari za Mazingira.

“Nataka kutoa rai kwa waandishi wa Habari wa magazeti, televisheni, bloggers namitandaoni kushiriki katika kampeni hii na mashindano haya tuzo na zawadi zitatolewakwenu,” amesema Jafo.

Ameiasa jamii na watanzania kwa ujumla kupanda miti rafiki kwa mazingirahususan ile ya matunda kulingana na jiografia ya maeneo yao kwa lengo la kuboreshana kuimarisha afya zao.Katika kampeni hii kubwa na ya kipekee jumla ya washindi 152 kutoka makundimbalimbali watapatikana na kupatiwa zawadi ikiwa ni pamoja na kupata fursa zakutembelea vivutio vya utalii ikiwemo mbuga za Wanyama hapa nchini


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages