WATU WENYEULEMAVU  WALILIA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO.

Na George Mwigulu KTPC,Katavi.

Chama cha Walemavu (CHAWATA) Mkoa wa Katavi kimeiomba serikali kupitia wizara ya afya maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto kupitia wataalamu wake wa afya kuhakikisha wanatoa elimu ya magonjwa ya mlipuko kwa watu wenyeulemavu kwani ni kama wamesahaulika huku magonjwa hayo yakiwatesa.

Akizungumza ofsini kwake na waadishi wa habari,Katibu wa chama hicho Godfrey Sadala alisema kuwa kwa muda mrefu jamii ya watu walemavu wamekosa kushirikishwa katika vikao vya kutolea elimu za afya,ambapo ni Mungu pekee ndiye anayewalinda dhidi ya magonjwa hayo hatari ya mlipuko.

Sadala amesema baadhi ya magonjwa yanayowatesa walemavu ni magonjwa ya kuharisha,matumbo pamoja na mafua makali  kutokana na kuwa walemavu wengi hutembea kwa namna ya kutambaa kwa kutumia mikono hivyo wanakuwa katika hatari ya kushika vitu vichafu kila wakati.

“ watu wenye walemavu wengi wanatambaa na wanakuwa kwenye mazingira hatari zaidi pale wanapokwenda msalani kwa sababu hata vyoo wanavyotumia ni vile ambavyo vinatumiwa na watu wengine ambapo kimsingi utavikuta vichafu sana” alisema Katibu huyo.

Katibu huyo wa chama cha walemavu alifafanua kuwa hali ni mbaya zaidi pale watu wenyeulemavu wanapokuwa wangonjwa na kuhudhuria katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma ya afya kwani kutokana na mazingira ya vituo hivyo vinawapa wakati mgumu zaidi hasa wanapokweda msalani.

Sadala ameiomba serikali kutilia mkazo  zaidi otolewaji wa elimu kwa walemavu,Kwani walemavu ni sehemu ya jamii ambapo pindi magonjwa ya mlipuko kama kipundupindu yanapotokea anayeathirika zaidi ni mtu mwenyeulemavu.

Aidha amebainisha kuwa kama chama cha walemavu mkoa wa Katavi wameshindwa kufanya vikao au mikutano yoyote na kuwaita wataalamu wa afya kwa ajili kutoa elimu ya kujikinga kwa sababumtu mlemavu unapomwita dhana iliyojengeka ni kuwa anakwenda kupatiwa msaada wa kifedha na wakati mwingine unakuwa kama usumbufu kwao.

Hivyo watalaamu wa kutoa huduma ya afya amewaomba kutembelea katika makazi yao moja kwa moja kuwaelimisha hasa kwa kuzingatia pia katika maeneo ya vijijini ambapo watu wengi walemavu wanapata mateso makubwa ya kiafya.Ambapo watapata ufahamu wa namna ya kujikinga na kuyatokomeza magonjwa hayo.

Mratibu wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko wa Hosptali teuli ya rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Taphinez Machibya alikiri kuwa magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara na kipundupindu kwa watu walemavu yanakuwa na changamoto kubwa yanapotokea.

Dkt Machibya amesema kuwa kuna juhudi mbalimbali ambazo kupitia wizara ya afya wamekuwa wakizifanya kuhakikisha watu hao wanakuwa salama.

Katika ugonjwa wa kuhara na kipundupindu wamekuwa wakitoa elimu kwa watu wenye ulemavu licha ya kuwa na changamoto ya kuwafikia kiharaka kutoka na baadhi ya jamii kuwa inawaficha.

Katika Kujikinga na Ugonjwa wa kipindupindu ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa kuhakikisha wanayatibu kwa dawa au kuyachemsha,Kunawa mikono kwa maji safi na salama na sabuni kila mara baada ya kutoka chooni ili kuepuka kula/kushika chakula huku mikono ikiwa michafu.

Licha ya kuzingatia usafi wamekuwa wakiishauri jamii kujenga choo angalau mita 30  kutoka kilipo chanzo cha maji pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi,Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa kuua bacteria aina ya Vibrio Cholera wanaosababisha ugonjwa wakipindupindu.

Aidha aliongeza kuwa kama Hospatali teuli ya rufaa ya Mkoa wa Katavi wanaompango kazi maalumu wa kuhudumia watu wenye ulemavu na wazee,Na hata pale wanapofikishwa hosptalini wanavyo vyumba maalumu vya kuwalaza.


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages