BUCHA LA WANYAPORI LA FUNGULIWA KATAVI.

 



Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma ZuberI Homera akizundua bucha ya nyama pori(Picha na George Mwigulu)


Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.

MKUU wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera amezindua bucha la kuuza nyama ya pori na kuwaasa wananchi kuacha na hata  kabisa vitendo vya ujangili vilivyokua vikitendeka katika mapori ya akiba ya wanyama pori na kwa wale wanaohitaji  nyama pori wa fuate  taratibu zilizowekwa kwa ajili ya upatikanaji wa nyama pori hiyo.




Muonekano wa Jengo la Bucha ya NyamaPori Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi(Picha na George Mwigulu)

MKUU wa Mkoa wa Katavi Komredi Juma Zuberi Homera amezindua bucha la kuuza nyama ya pori na kuwaasa wananchi kuacha na hata  kabisa vitendo vya ujangili vilivyokua vikitendeka katika mapori ya akiba ya wanyama pori na kwa wale wanaohitaji  nyama pori wa fuate  taratibu zilizowekwa kwa ajili ya upatikanaji wa nyama pori hiyo.

Wazee wa Kisilamu wapongeza hatua hiyo ya uzinduzi   bucha hiyo ya wanyama pori na wamesema kuwa toka Dunia iundwe walikuwa haja wahi kufutulishwa kwa nyama ya pori isipokuwa kwenye mfungo huu ulioanza   wa  mwezi  mtukufu wa ramadhani.

Akizindua Bucha hilo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homea amempongeza mwekezaji kwa kuweza kufuata taratibu na kufanikiwa kufungua bucha hilo sambamba na mmilikiwa wa jengo lililopo bucha hilo la kuuza nyama hiyo ya  pori kwa kutengenea jengo la kisasa na kuwa miongoni mwa majengo mazuri ya kisasa yaliyopo Mkoa wa Katavi.

Mbali na hayo Komredi Homera amesema kuwa kufunguliwa kwa bucha hilo la nyama ya pori  hapa Katavi na hata nchini nzima kwa ujumla ni muendelezo wa kumuenzi kwa vitendo aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Joseph Magufuli katika tamko alilolitoa Oktoba 10,2019 katika ziara yake aliyoifanya Mkoa wa Katavi kwa kutaka kuanzishwa kwa mabucha ya nyama ya pori hapa nchini.

"Aliyekuwa Rais watu Hayari Dk Magufuli alipofanya ziara ya kikazi hapa Mkoani kwetu alitoa tamko la kuanzishwa kwa mabucha ya nyama pori hivyo leo tumetimiza agizo hilo na hasa ukizingatia agizo hilo alilitoa kwa mara ya kwanza akiwa ziarani mkoani kwetu hivyo ninaimani tumemuenzi kwa vitendo"alifafanua Mkuu wa Mkoa Homera.



Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Comrade Juma Zuberi Homera akitoa huduma ya kumpimia na kumuuzia nyama pori Mkuu wa wilaya ya Mpanda,Bi Jamila Yusuph.

Aidha ameongeza kuwa badala ya kulinda  wanyama tu wananchi wamepata fursa ya kula nyama ila kwa kufuata sheria na utaratibu na sio kutumia fursa hii kuendeleza ujangili kwa kuwauwa wanyama porini na kusingizia wamenuna katika bucha linalouza nyama pori.

 Amesema kuwa bei ya nyama pori itakuwa ikiuzwa kwa bei ya TSHS 8000  kwa kilo bila kujari nia aina gani iwe nyati ,swala isha ,mbawala  kongoni. nyemela na pofu zote zinauzwa kwa bei hiyo kwa kilo na nyama hizo za pori zitakuwa zinauzwa mara tatu kwa wiki katika kipindi hiki cha masika kiangazi zitakuwa zikiuzwa kila siku na watu watakula nyama hizo mpaka watachoka wenyewe

Kwa upande wake Meneja wa Pori la Akiba Rukwa {TAWA} Baraka Balagaye alisema kuwa kwa yoyote ambaye anataka kufungua bucha la nyama pori wao kama wasimamizi wa mapori ya akiba wapo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kufungua mabucha mengi ya kuuza nyama ya pori.



Mkuu wa Mkoa wa Katavi (wa kwanza kushoto) akikagua baadhi ya nyama pori waliohifadhiwa kwenye jokofu.

Nae Mmilikiwa bucha hilo la kuuza nyama pori Vedasto Magaba aliwashukuru Viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Juma Homera kwa kufanikisha yeye kuweza kufungua bucha hilo bila kuwa sahau TAWA wanaosimamia mapori ya akiba na kutoa vibali vya kuwinda wanyama hao kwa ushirikiano waliompatika katika kufanikisha upatikanaji wa nyama na kufungua bucha hilo.

Sambamba na hayo naye Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidary Summry alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa namna anavyosukuma maendeleo ya Mkoa wa Katavi kwa kasi kubwa na matokeo chanya yanaonekana ikiwepo uzinduzi wa bucha la kuuza nyama pori alilolizindua.




Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kununu nyama pori baada ya bucha hiyo kuzinduliwa.

Nao baadhi ya wanachi waliokuwepo katika uzinduzi huo akiwepo Shaban Bakari alisema kuwa wamefurahishwa na kuzinduliwa kwa bucha hilo la kuuza nyama pori kwani hawakuwahi kutegemea kutokea kwa fursa ya kuuza nyama pori na leo kwa mara ya kwanza wanaanza mwezi mtukufu kwa kufuturishwa nyama ya pori.

Katika bucha hilo lililozinduliwa na Mkuu huyo wa Mkoa lenye maneno Kula nyama pori kwa afya yako,kilo moja ya nyama itapatika kwa bei ya shilingi elfu 8 baada ya mkuu wa Mkoa kuzungumza na mmiliki wa bucha hilo aliyetaka nyama hiyo kuuzwa kwa bei ya shilingi 10,000 kwa kilo moja.








Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages