
Kituo cha Radio cha pamoja FM kimeanza kampeni ya kugawa vifaa vya kujikinga Na ugonjwa wa UVIKO-19 sambamba na kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi katika manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

Wanafunzi hawajatajwa na serikali kwenye mpango wa kupewa chanjo na serikali ambapo ni kundi lenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo.

Katika uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika katika shule ya sekondari Mwangaza, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Haidary Sumry amekipongeza kituo hicho cha radio cha Pamoja Fm kwa kubuni njia ambayo itawasaidia wanafunzi kujikinga na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza.
Kampeni hiyo itaendelea jumatano,Agost 18 mwaka huu katika shule ya sekondari Rungwa iliyopo Kata ya Kazima manispaa ya Mpanda Mkoani hapa.
