KATAVI WAFANYA ZOEZI LA  UTAYARI  WA UOKOAJI WA AJARI YA NDEGE

 


Na Walter Mguluchuma

       Katavi

Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania Kanda ya Magharibi  kwa kushirikiana na  vyombo vya ulinzi vya Mkoa wa Katavi wamefanya zoezi la  utayari  wa  ukoaji wa  ajari ya ndege   pindi  ajari  itakapo kuwa imetokea  kwa mafanikio makubwa




Kamanda wa Polisi wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi Kaster Ngonyani   amesema  zoezi hilo linawajengea uwezo mkubwa   sana  endapo itakapokuwa ajari ya ndege   imetokea kwa   kuweza  kufika  kwa haraka sana kwenye eneo la tukio kama walivofanya kwenye zoezi hilo  kwa bidii wakiwa na wafanyakazi wa  uwanja wa ndege wa Mpanda .

Amesisitiza kuwa  hilo lilofanyika ni zoezi tuu sio kwamba kuna  ajari  ya ndege ambayo  imeanguka kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda  bali ni zoezi tuu la utayari

Kaimu  Kamanda wa  jeshi la zima moto na uokoaji wa Mkoa wa Katavi  Liliana  Joshuwana  amesema walikuwa katika  uwanja wa ndege wa Mpanda  kwa ajiri ya zoezi la utayari  kwa ajiri ya ndege iliyodondoka Ikiwa na abiria 30 lakini hamna kifo kilichotokea  wote walikuwa majeruhi  zoezi hilo  sio kwamba ndege  ilikuwa  imeanguka  kiuwalisia  ni zoezi la utayari  kwa vyombo vyote  vya ulinzi na usalama .




Amewatowa  hofu wananchi wa Mkoa wa Katavi na Wanzania kuwa hilo likuwa ni zoezi la utayari  wa  uokoaji  na sio ajari  ya ndege  kiuhalisia .

Meneja  wa viwanja  vya   ndege  Kanda ya Magharibi   Fadhili Maginema amebainisha kuwa  wafanya zoezi la  utayari  wa ajari ya ndege kama ambavyo  matakwa ya kisheria na  kikanuni   ya mdhibiti  wa  mamlaka  ya  anga Tanzania  ambayo inawahitaji wafanye  zoezi hilo  la utayari kila baada ya miaka miwili .

Amefafanua kuwa zoezi  hilo limehusisha  taasisi zote  ambazo zipo  kwenye maokozi  yaani Polisi ,jeshi la zima moto , Jeshi la wananchi wa Tanzania ,  usalama wa Taifa  na Mahospitali yote yaliyokatika Mkoa wa Katavi  na mamlaka  ya viwanja vya ndege  wanachoangali  ni   namna ya kujilinda wakati wa ajari  kwa kila taasisi kujua wajibu wao wanaotakiwa kufanya pindi ajari ikitokea .

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages