Mzee Exvery Mwanamahenge mkazi wa kijiji cha Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefanikiwa kuweka akiba fedha za uhawilishaji kutoka Tasaf hadi kufikia hatua ya kununua mifugo ya ng'ombe wawili aliowazalisha hadi kufikia nane.
WALENGWA
TASAF MLELE WAOMBWA KUZINGATIA MATUMIZI BORA YA FEDHA.
Na
Walter Mguluchuma ,Mlele.
Wanufaika
wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wameombwa
walengwa wote kuonesha usubutu wa kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha kidogo
wanazopata kwa ajili ya maendeleo.
Fedha
wanazopata wameaswa kuzingatia kwenye matumizi kwenye kuanzisha miradi
mbalimbali ikiwemo ufugaji wa mifugo ya Ng'ombe,Mbuzi na Kodoo,Kilimo na ujenzi
wa nyumba kwa ajili ya makazi bora.
Hayo
yamesemwa jana na Mratibu wa Tasaf Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Graceanna
Msemakweli wakati wa zoezi la tathimini ya mafanikio waliyoyapata baada ya
uwahuhishaji fedha kwa walengwa katika kjjiji cha Ilunde kama wanatumia kwa
malengo yaliyokusudiwa.
Mratibu
huyo aliweka wazi kuwa kuna baadhi ya walengwa wamekuwa na tabia ya kuona fedha
hizo kuwa ni kidogo sana,Lakini alisisitiza kuwa kuna walengwa wengine
zimewasaidia fedha hizo kusomesha watoto shule,kuwapatia chakula angalau milo
mitatu kutwa pamoja na kupata matibabu ya afya.
"Ukweli
ni kuwa Tasaf imefanikiwa kupunguza umasikini kwa kiasi kikubwa kwa watu ambao ni
walengwa wa mpango...kwahiyo mfuko huo haupaswi kubezwa kwa namna yoyote ile
kwani kufanya hivyo ni kutokuonesha uzalendo kwa serikali ambayo inafanya
juhudi kubwa ya kumkwamua mwananchi kwenye umasikini"alisema Granceanna
Aidha
Granceanna alifafanua kuwa jumla ya vijijini vinne kati ya vijijini 18 katika
halmashauri ya wilaya ya Mlele yenye Kata sita viko kwenye mpango ambapo
walengwa 267 wako kwenye mpango wa kunufaika na uhuhiswaji.
Mzee
Exvery Mwanamahenge Mkazi wa kijiji cha Ilunde mnufaika wa Tasaf alisema kuwa
fedha alizopata zimemsaidia kujiwekea akiba hadi kufikia hatua ya kununua
ng'ombe wawili na kuwazalisha hadi kufikia nane.
Mwanamahenge
alisema kuwa jumla ya fedha Tsh 35,000/= kuhuwishwa kutoka Tasaf ambazo pia
zimemwezesha kulima shamba la ekari tatu za zao la mpunga na kufanikiwa kuvuna
gunia 35 alizoziuza kisha kununulia mifugo ya ng'ombe.
Naye
Mariam Hassain mkazi wa kijiji hicho alisema kuwa naye amekuwa akipata
uhuwishwaji wa fedha Tsh 35,000/= kutoka Tasaf zilizomwezesha kuweka mizinga
kadhaa ya nyuki ambapo baada ya kulina asali hiyo na kuuza imemganikisha
kuongeza mtaji wa uwekaji wa mizinga ya nyuki kufikia idadi ya mia mbili ya
nyuki.
Mariam
aliongeza kuwa licha ya Tasaf kuwa mkombozi wa kujikwamua kwenye maisha magumu
pia wamepokea ushauri wa mratibu wa Tasaf wilaya ya Mlele kwa kujenga nidhamu
ya matumizi ya fedha hizo kwa masirahi ya familia zao,Pia amewashauri wanufaika
wenzie kuzingatia ushauri huo.
MWISHO.