Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Dk Godwin Mollel (kwenye wa kwanza kutoka kushoto) akiwa na mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini Mkoa wa Katavi Sebastian Kapufi.
Na Mwandishi Wetu KTPC,Mpanda.
Mbunge wa jimbo la
Mpanda mjini Mkoa wa Katavi Sebastian Kapufi amechagia kiasi cha shilingi
milioni 10 kupitia mfuko wa jimbo itakayosaidia uzalishaji wa vifaa tiba
katika hosptali teule ya rufaa ya mkoa huo ambapo kwa kufanya hivyo kutasaidia
hosptali hiyo kuondokana na uhaba wa vifaa tiba.
Sebastian Kapufi
ambaye ni mbunge wa jimbo Mpanda mjini amefikia uamuzi huo wakati wa
ziara ya siku moja iliyofanywa na naibu waziri wa afya na maendeleo ya jamii
jinsia wazee na watoto Dkt Godwin Mollel mkoani hapo,ambapo baada ya
kusikiliza kati ya changamoto ambazo zinaikabili hosptali hiyo ya uhaba wa
vifaa tiba aliamua kuchangia fedha hizo.
"Tusiende
kuchangia pekee kwenye misimba kwa watu walio kwisha kufa tayari badala ya kuja
kuchangia kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu" alisema Kapufi
Licha ya kuchangia
kiasi hicho cha fedha alimuomba naibu waziri wa afya na maendeleo ya jamii
jinsi wazee na watoto Dkt Godwin Mollel kuongeza ujenzi wa idadi ya vituo
vya afya katika kata ya Nsemlwa ambayo inawatu 14,000 pamoja na Kata ya
Kakese wakazi 18,000 sambamba na Kata ya Mwamkuru ambazo zote kwa pamoja
zinaidadi kubwa ya watu ambapo inafaa kupatiwa vituo vya afya.
Kapufi alisema
"Ninatambua kuwa kwa awamu ya kwanza tuliweza kupata kituo kimoja cha Afya
cha Ilembo kilichopo manispaa ya Mpanda,hivyo ninashukuru kwa kupatikana kwa
kituo hicho kwani kusema asante ni kuomba tena,Na pindi maboresho yanafanyika
ya kuongeza vituo vya afya nasi tunaomba kupatiwa vituo vipya vya afya" .
Aidha ameomba suala la
kuongezwa kwa watumishi wa afya katika hosptali teule ya rufaa ya mkoa wa
Katavi licha ya kuwa changamoto zilizopa anazifahamu lakini kuna kila umuhimu
wa kutilia mkazo suala hilo.
"...haya tumekuwa
tukiyasema huko ni vema umekuja site na kuyaona maana wataalamu wanasema mara
nyingi watu huamini kwa yale wanayoyaona,Na wewe umeendelea kuona uchakavu wa
majengo pamoja na upungufu wa wataalamu wa afya" alisisitiza mbunge huyo.
Pia alieza kuwa
kushindwa kukamilika kwa wakati ujenzi wa hosptali mpya ya rufaa mkoani humo
unatokana na kupokea uhaba wa fedha,ambapo wameweza kupokea kiasi cha bilioni 3
ikilinganishwa na bajeti ya ujezi huo ambao unagharimu bilioni 9 hadi
kukamilika,Hivyo amemuomba naibu waziri kulishughurikia tatizo hilo.
Dkt Godwin
Mollel,Naibu waziri wa afya na maendeleo ya jamii jinsi wazee na watoto katika
kuhakikisha suala la uhaba wa vifaa tiba linakwisha kwenye hosptali hiyo
kutokana na uzalendo,welendi,ufanisi na ubunifu wa Mfamasia wa Hosptali Teule
ya rufaa mkoa wa Katavi Furahisha Chaula alimteua kwenda kwenye hosptal
ya rufaa ya mkoa wa Mbeya kwa mafunzo ya wiki mbili kwa ajili ya kujifunza.
Vilevile suala la
uhaba wa watumishi wa afya naibu waziri alisema serikali kupitia wizara yake
wanashughurikia changamoto hiyo,Huku akiutaka uongozi pia wa hosptali hiyo
kuongeza bajeti yake ya ununuzi wa madawa ili kuondoa uhaba wa dawa
unaosababisha kupungua kwa makusanyo ya mapato ya fedha.
Dkt Yustina
Tzeba,Mganga Mkuu wa Hosptali teule ya rufaa ya Mkoa wa Katavi amesema
wamefakia kupata mafanikio ya kuboresha huduma kwa kuanzisha huduma ya Fast
track(huduma za haraka),duka la dawa ,X-ray ya kisasa kwa ajili ya kuboresha
huduma,Pia wamefanikiwa kuhamasisha uandikishwaji wa bima na huduma za
kuandikisha iCHF zimefunguliwa hosptalini hapo.
Pamoja na hayo
wamefanikiwa kuanzisha vitengo vipya vya dharura,lishe,uangalizi maalum kwa
wagonjwa mahututi na maandalizi ya kitengo cha utengano shufaa tayari mtaalam
amepatikana na kuajiliwa kwa mkataba