Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Mahakama ya Mwanzo ya Mpanda Mjini imewahukumu watu wawili kwenda jela kifungo cha miezi miwili,mmoja kifungo cha kutumikia jamii kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuiba kuku na kumtowa manyoya yake yote nyumbani kwa baba mkwe wa mshitakiwa wa pili.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo ya Mpanda Mjini David Mbembela baada ya washitakiwa hao wote wawili kukiri shitaka Mahakamani hapo baada ya kuwa wamesomewa mashitaka Mahamani hapo .
Watuhao waliohukumiwa Mahakamani hapo katika kesi hiyo iliyowasisimua wakazi wa Mji wa Mpanda kutokana na tukio hilo ni Crispin Peter na Richald Elias wote wakazi wa eneo la Kampuni Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi .
Washitakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Januari 8 mwaka huu majira ya saa tano usiku huko katika eneo la Kampuni Kata ya Misunkumilo nyumbani kwa Meshack Siprian ambae ndie alikuwa mwenye kuku hiyo .
Katika tukio hilo watuhumiwa hao walidaiwa kuwa baada ya kuwa wamefika kwenye nyumba ya mwenye kuku huyo ambae ni baba mkwe wa mshitakiwa wapili waliiba kuku huyo na kumchinja na kisha walimwachia manyonya mwenye kuku huyo kwenye nyumba yake ambapo asubuhi baada ya kuamka alikuta kuku wake akiwa hayupo na aliambulia kuona manyonya ya kuku tuu.
Washitakiwa hao walipo somewa mshitaka yaliyokuwa yameandaliwa kwenye hati ya mashitaka ya kutoka jeshi la polisi Wilaya ya Mpanda mbele ya Hakimu David Mbembela alikuwa akisikiliza kesi hiyo kwa kushirikiana na wazee wa baraza washitakiwa hao walikiri kutenda kosa hilo na waliweza kukubali kidhibiti cha manyonya ya kuku yaliyoletwa Mahakamani hapo kama ushahidi na walikubali kuwa manyonya hayo ni ya kuku ambae walimwiba na kumchinja nymbani kwa Meshack Spirian .
Baada ya washitakiwa hao kukiri mashitaka hayo ambayo walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la wizi kinyume cha kifungu cha sheria Namba 265 cha Kanuni ya adhabu sura ya 16 hivyo Hakimu Mbembela alitowa nafasi kwa Askari Sajenti Abiyud ambae anasimamia amari za Mahakama kama analo jambo lolote la kuiambia Mahakama .
Ambapo aliiambia Mahakama kuwa jeshi la polisi halina kumbukumbu zozote zile ambazo zinaonyesha kuwa washitakiwa hao waliwahi kutenda kosa jingine lolote la wizi kama huo .
Katika utetezi wake mshitakiwa wa kwanza Crispin Peter aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa kosa hilo kwake ni la kwanza na pia anafamilia yake ya watoto wanne inamtegemea yeye na mke wake ameisha mkimbia na kumwancha watoto .
Mshitakiwa wapili aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa kuna familia ya watoto ambayo inamtegemea na mke na pia analotatizo la ulemavu wa mkono wake wa kulia.
Akisoma hukumu hiyo ambayo iliungwa mkono na wazee wote wawili wa Baraza Hakimu Mbembela aliiambia Mahakama kuwa Mahakama imewatia hatiani washitakiwa wote wawili baada ya kukiri kosa lao hivy Mahakama imezingatia kuwa kwa kuwa kosa hilo walilofanya ni mara yao ya kwanza na thamani yake ya kuku ni ndogo ya tshs 15,000.
Kwa hiyo mshitakiwa wa kwanza anahukumiwa kulipa faini ya shilingi 30,000 au kwenda jela kifungo cha mwezi mmoja na aliweza kukupa kwenda jela baada ya kuwa amelipa faini hiyo .
Mshitakiwa namba mbili alihukumiwa kwa kifungu cha sheria cha 3 cha sheria ya huduma za jamii Namba 6 ya mwaka 2002 ambapo alihukumiwa Adhabu ya kutumikia jamii kwa kufanya kazi kwa muda wa miezi miwili .
Mbembela alieleza kuwa adhabu hiyo ya kutumikia jamii Mahakama imeona itowe kwa kuwa mshitakiwa anatatizo la ulemavu wa mkono na pia ni sehemu ya kupunguza msongamano kwenye gereza na mshitakiwa kupata nafasi ya kutumikia adhabu kisha kurudi kuishi na familia yake badala ya kuwa gerezani .