AFARIKI DUNIA KWA KUMEZWA NA MAJI



Kamishina Msaidizi wa Jeshi la ZimaMoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi Reginal Kaombwe

Na Neema Hussein KTPC, KATAVI

MTOTO aliyefahamika kwa jina la Abbas Masoud mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi saba amefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji.

Tukio hilo limetoke octoba 10,2020 katika mtaa wa migazini kata ya nsemulwa halmashauri ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi ambapo mtoto huyo hawakuweza kumuona kwa muda mrefu katika mazingira ya nyumbani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamishina msaidizi wa Jeshi la zima Moto na uokoaji Mkoani humo Regina Kaombwe alikili kupokea taarifa hizo na kuwataka wananchi ambao hawajafumika visima wafunike mara moja.

Alisema wataanza kuchukuwa hatua endapo watabaini Kuna mtu ambaye hajafunika kisima chake ikiwemo kumkamata na kumfikisha mahakamani akiamini ndio njia sahihi ya kuepukana na majanga ya watoto au watuwazima kupoteza maisha kwa njia hiyo.

Akizungumza na nipashe babu wa marehemu Deo Mbogo alisema mtoto huyo alikuwa ni mgeni ambaye alikuja na mama yake kufuatia ugomvi wa kifamilia baina ya wazazi wa mtoto huyo.

"Huyu binti mi mwijukuu wangu waligombana na mume wake akawa amekimbilia huku kutafta suluhisho la ugomvi mkubwa ulikua ni huyo mtoto ambapo mama yake alitaka mtoto abaki na baba yake ila mke wangu akawashauri huyu mtoto ni mdogo huwezi kumuacha na baba yake hawakuweza kuelewa ikabidi awambie waende polisi  sasa wakati wakiendelea na kesi ambapo waliambiwa warudi siku inayofuata baba mtu akaondoka nyuma likatokea hili," alisema Mbogo.

Alisema kabla ya kifo cha mtoto huyo mama yake alikuwa anafua mazingira jirani na kilipo kisima hicho hivyo mtoto huyo alikuwa akimuona mama yake anavyokwenda kuchota maji ndani ya kisima hicho.

Alisema wao wakiwa ndani ulipita muda pasipo kumuona mtoto huyo ndipo walipo anza kumtafta katika mazingira ya njee na ndani ya nyumba badaye mama yake alikwenda kufunua ndani ya kisima na kumkuta mtoto wake kaisha fariki ndipo taratibu zingine ziliendelea

Myenyekiti wa mtaa huo Ahamad Kahena alisema ni mara ya tatu sasa kutokea kwa tukio kama hilo katika mtaa wake hivyo amewataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao pia kawasisitiza kufunika na kujengea visima vyao.

 

 


 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages