Katibu wa Chama cha Waadishi wa Habari Mkoa wa Katavi,Paschal Katona akikabidhiwa hati ya pongezi kwa chama cha waadishi wa habari (KTPC) kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Mkoa wa Katavi,Fuljensia Kapama(wa nne kwenye picha kutoka kushoto )
Na Mwandishi wetu KTPC,Katavi.
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Katavi katika kutambua juhudi za waadishi wa habari Mkoani humo kimetoa hati mbalimbali za pongezi ikiwa ni moja ya kutambua mchango unaotolewa na waadishi wa habari kwenye umoja huo.
Chama cha waadishi wa habari Mkoa wa Katavi (KTPC) kimetunukiwa hati ya pongezi kutokana na kazi kubwa inayoifanya ya kuhabarisha umma kupitia wanachama wake ambapo ni waadishi wa habari na wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Mwandishi wa Habari wa Site Tv ya Mkoa wa Katavi,Swaumu Katanbo akipokea hati ya pongezi kwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Katavi,Fuljensia Kapama ( kwenye picha wa tatu kutoka kulia)
Akipokea hati hiyo Katibu wa KTPC na mwandishi wa Channel Ten Mkoa wa Katavi, Paschal Katona ameushukuru kwa dhati umoja huo kwa kutambua mchango unaotolewa na KTPC kwani hati hiyo ni heshima kubwa kama taasisi imetunukiwa.
Katona amesema kuwa kwa niaba ya waadishi wa habari anaahidi kufanya kazi zaidi na Umoja wa Wanawake Tazania Mkoa wa Katavi na jamii yote ya wanaKatavi ili kuwa sehemu ya chachu ya maendeleo kwa wanawake wote na Mkoa kwa ujumla.
Mwandishi wa Habari wa Channel Ten Mkoa wa Katavi akipokea hati ya pongezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake(UWT) Mkoa wa Katavi Fuljensia Kapama( wa pili kutoka kulia)
Amewaondoa shaka UWT kuwa suala la maadili litazingatiwa zaidi kwenye uandishi wa habari zote zinazowahusu wanawake ili kuepuka kuwa sehemu ya kuwazalilisha na kuwashusha katika juhudi zinazofanywa na umoja huo wa kumkwamua mwanamke kutoka kwenye unyonge na kuwa wenye nguvu na uwezo wa kushika nafasi kwenye ngazi za utawala.
Site Digital Media ni miongoni wa kampuni ya chombo cha habari ya Mkoa wa Katavi iliyotunukiwa o chati za pongenzi sambamba na Kitu cha habari cha Channel Ten