WAHUDUMA WA AFYA NGAZI YA JAMII WAPINGWA MSASA KUTOKOMEZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi (RMO) Dkt Omary Sukari akifungua semina ya wahudumu wa afya ngazi ya Jamii Mkoani humo.

Na Ezrom Mahanga KTPC,Katavi.

Watoto 581 na Wanawake 57 wamefariki dunia kutokana na vifo vya uzazi kwa takwimu ya mwaka 2017  nchini.

Kutokana na vifo hivyo Mkoa  wa Katavi unafanya kila jitihanda za kuhakikisha wanapunguza vifo hivyo vitokanavyo na uzazi ili wanafamilia wafurahie suala la uzazi.

Serikali ya Mkoa wa Katavi inaendesha semina ya siku 28 kwa wahudumu ngazi ya Jamii 130 kutoka halmashauri tano za Mkoa huo ili kwenda sambamba na kukabiliana na tatizo hilo.


Baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii waliohudhuria kwenye semina ya kupambana na vifa vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi

Akifungua semina hiyo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt Omary Sukari amewaomba wahudumu hao wanaopata kupata semina hiyo kuwa wanakwenda kutoa elimu ya uzazi  wa mpango pamoja na kuhusu suala la udumavu unaosababishwa na kukosa lishe.


Baadhi ya wahudumu wa afya ngazi ya Jamii wakiendelea na mafunzo ya semina yao.

Kutolewa kwa semina hiyo kunalenga kupambana  na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kama alivyobainisha Mratibu wa huduma za afya ngazi ya Jamii  Wizara ya Afya Dkt Meshack Chinyuli.

Aidha baadhi ya wahudumu walioshiriki semina hiyo wameahidi kuwa mabalozi wa kutokomeza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi. 

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages