Na George Mwigulu KTPC,Katavi.
Wakazi wa mkoa wa Katavi wametakiwa kuachana na fikra potofu kuwa ugonjwa wa kipindupindu husababishwa na kulogwa yaani imani za kishirikina.
Hii ni kutokana na kuwa jamii mkoani humo hasa ya vijijini inayokaliwa
na wakulima na wafungaji kujihusisha katika kulipiza visasi na kusababisha vifo
baada ya kwenda kwa waganga wa kienyeji kupiga ramli ambazo ni choganishi
wanapokuwa wagonjwa wakidhania huenda wamelengwa.
Rai hiyo imetolewa jana na mratibu wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko wa Hosptali teuli ya rufaa ya Mkoa wa Katavi Dkt Taphinez Machibya alipokuwa akizungumza na Gazeti la Majira ofisini kwake,ambapo alisema jamii isipotambua maana ya ugonjwa wa kipindupindu,chanzo chake,dalili zake,athari pamoja na kushindwa kuchukua hatua ya kudhibiti ugonjwa huo wataagamia.
Uharibifu wa mazingira unasababishwa na mafuriko ya mvua yaweza kuwa chanzo wa magonjwa ya mlipuko kama vile ugonjwa wa Kipindupindu,ambapi jamii inapaswa kuchua tahadhari ya kujikinga zaidi. |
Alifafanua kuwa mabaki ya matapishi au kinyesi yanayobaki na kuguswa na
mtu mwingine pengine yakachukuliwa na nzi kutoka eneo moja hadi jingine hasa
kwa kugusa vyombo vya maji/chakula,chakula chenyewe au mtu mwenyewe akagusa
mgonjwa atakuwa kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa.
Aliweka wazi kuwa ugonjwa wa kipindupindu unaweza kutokea ni msimu wa
kutupwa takataka hovyo,kuiva magunda mengi pamoja na kujisaidia nje ya mashimo
ya vyoo hasa kwenye mikusanyiko ya watu wengi.Hivyo aliwataka wananchi kujenga
vyoo na kuvitumia kwa usahihi.
Dkt Majibya aliwaambia wananchi kuwa pindi wanatakapo kuwa wanaona
dalili za homa,kutapika,uchovu na kuharisha majimaji ya rangi inayofanana na
maji yaliyooshewa mchele inawapasa kutoa taarifa kwenye vituo vya afya ili
hatua ziweze kuchukuliwa.
Aidha jamii inapaswa kutambua kuwa athari zinazoweza kutokea ni pamoja
na kuwa na vifo kutokea kwa wingi ndani ya muda mfupi na kupoteza taifa
rasilimali watu,familia kuwa na mzingo wa kuelea watoto yatima waliofiwa na
wazazi wao.
Athali nyingine mratibu huyo alisema ni upotevu wa rasilimali fedha kwa
sababu ugonjwa ambao unahitaji mapambano makali ndani ya muda mfupi,kwahiyo
jamii na serikali kutumia bajeti kubwa ili kuzuia kasi ya maabukizi.
Hivyo aliwaasa jamii kwa ujumla kuzingatia kufanya usafi kwenye makazi
yao pamoja na kuhifadhi vizuri taka mwili hasa taka zitokanazo na choo na
kunawa mikono kwa maji safi na salama na wala sio kuwa na dhana potofu za imani
za kishirikina.
Utumiaji wa maji yasiyochemshwa husababisha ugonjwa wa kipindupindu,hivyo jamii inapaswa kuchesha maji au kuyatibu kabla ya matumizi ya kunywa. |
Nao baadhi ya wananchi wa mkoa huo Alex Mwandu mkazi wa mtaa wa
Nsemlwa alisema serikali inapaswa kutoa zaidi elimu ya magonjwa ya mlipoko.
Mwandu aliongeza kuwa elima kama itatolewa kwenye jamii hasa ya vijijini
itasaidia watu kuchukua tahadhari za mapema za kujilinda ikiwa pamoja na
kuachana na imani potofu za kuhusu magonjwa.
Aisha Hassain Mkazi wa mtaa wa Misukumilo manispaa ya Mpanda mkoani humo
alisema kuwa uwepo wa ongezeko la vituo vya afya na zahanati vijijini itasaidia
kutokomeza magonjwa ya mlipuko kwenye jamii.
Alisema kuwa zahanati pamoja na vituo hivyo vya afya kutokana na kuwa na
wataalamu wa afya vimewasaidi wananchi hata pale wanapokuwa wagonjwa kupata
matibabu sitahiki na kuyatokomeza magonjwa hayo.