![]() |
Muonekano wa bustani za mboga mboga kando ya mto kasimba hali ambayo inatishia usalama wa mto huo |
Na Mwandishi wetu
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya
Mpanda katika Mkoa wa Katavi wamelalanikia uhalibifu wa mto Kasimba ambao ni chanzo cha maji
unavyoharibiwa kwa kufanyiwa shughuli za
kilimo huku mamlaka
zikishindwa kuchukua hatua zozote za haraka za kuunusuru mto huo.
Hali ilivyo kwa sasa kwenye mto kasimba ambao wananchi wameanza kufanya shughuli za kibinadamu hususani kilimo cha bustani za mboga mboga kwenye kingo za mto huo.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mpanda katika Mkoa wa Katavi wamelalamikia uhalibifu wa mto Kasimba ambao ni chanzo cha maji unavyoharibiwa kwa kufanyiwa shughuli za kilimo huku mamlaka zikishindwa kuchukua hatua zozote za haraka za kuunusuru mto huo.
Wananchi wamedai kuwa endapo mamlaka hazitachukua hatua za haraka upo uwezekano mkubwa wa chanzo hicho cha mto Kasimba unaounganisha barabara muhimu ya kutoka kati kati ya Mji wa Mpanda na barabara ya kwenda Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Selemani Tengeneza mkazi wa Mtaa wa Kasimba amesema eneo hilo limekuwa ni kawaida wala si jambo geni kwa wananchi kufanya shughuli za kilimo na za kibinadamu kwani wamekuwa wakilima bustani za mboga mboga na kupanda mahindi kwenye chanzo cha mto huoAmeiomba Serikali kuchukua hatua sitahiki za haraka kunusuru
chanzo hicho cha mto ambacho kimekuwepo kwa muda mrefu sasa kuliko kukiacha
kikiendelea kuhalibiwa huku uwezekano wa
kukinusuru upo unawzekana .
Salome John ameeleza kuwa hapo
zamani ilikuwa ni marufuku kabisa kwa wananchi
kufanya shughuli zozote za kilimo wala za kibinadamu lakini wanashangaa
miaka ya hivi karibuni watu kuachwa wakiendelea na shughuli za kilimo cha bustani.