HALMASHAURI YA NSIMBO KUONGEZA UKUSANYAJI WA MAPATO MARA DUFU

Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Charles Halawa wakiwa katika picha ya Pamoja nje ya Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Chalinze 


Na Alex Ngereza-Pwani

Madiwami katika halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wamesema kuwa halmashauri ya Nsimbo itakuwa miongoni mwa halmsahauri zinazokusanya mapato kwa wingi katika mkoa wa Katavi ili kuisaidia halmashauri kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe akitoa neno kwa Uongozi wa Halmashauri ya Chalinze katika ziara ya Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo kwenye Halmashauri ya Chalinze

Madiwami katika halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi wamesema kuwa halmashauri ya Nsimbo itakuwa miongoni mwa halmsahauri zinazokusanya mapato kwa wingi katika mkoa wa Katavi  ili kuisaidia halmashauri kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Halawa Malendeja amesema Ziara hiyo inaenda kuleta mafanikio makubwa kwenye halmashauri kutokana na kufika eneo sahihi la kujifunza na hitaji lao la namna ya ukusanyaji wa mapato pamoja na shughuli za kiutawala

Madiwani kutoka halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi walipotembelea Soko la Kisasa la Chalinze kwenye ziara hiyo

Diwani wa kata ya mtapenda Eliezeli Fyula amesema kwasasa wanaenda kufanya kazi ambayo itakuwa na mafanikio makubwa na ziara hiyo inaenda kuleta tija kwa wananchi wa Halmashauri ya Nsimbo katika eneo la ukusanyaji wa Mapato.

Diwani wa Viti maalumu kutoka Kata ya Itenka Nesta Masebo amesema kupitia ziara hiyo ya kutembelea Halmashauri ya Chalizwe wameongezewa maarifa na ujuzi juu ya kubuni vyanzo vingi vya Mapato ambavyo vitaisadia halmashauri ya Nsimbo kuwa katika ukusanyaji wa Mapato.

Mbunge wa Jimbo la Nsimbo,Anna Lupembe akiwa na Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo walipotembelea Kituo cha Redio Chalinze

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nsimbo Anna Lupembe amesema lengo Kuu la Madiwani kwenda Chalinze na Tanga nikujifunza kwa halmashauri iliyofanikiwa kimapato na Kiutawala ili kuisaidia Halmashauri ya Nsimbo kubuni vyanzo vya Mapato na namna bora ya kukusanya mapato kwenye vyanzo hivyo.

Lupembe amesema halmashauri ya Chalinze Muundo wa Kiutawala inafanana nayo kwa maana hiyo wameona ni vyema kwenda halmashauri ambayo wanaendana nayo kiutawala pamoja na halmashauri hiyo kuwa na ukusanyaji Mkubwa wa makusanyo ambayo yanafikia zaidi ya bilioni 15 hii ni sababu iliyowafanya kwenda kwenye Halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Nsimbo  Michael Kasanga,akiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashari ya Chalinze wakati wa ziara hiyo.

Afisa Utumishi wa Nsimbo Aldof Simindu amewaomba Madiwani kutumia ziara hiyo kwa ajili ya kuboresha na kuimairisha ukusanyaji wa mapato na kuendelea kubuni vyanzo vya mapato ili kushindana na Halmashauri zilizoendelea kama Chalinze.

Katika ziara hiyo Madiwani wametembelea Mradi wa radio Halmashauri ya Chalinze wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 102, Mradi wa soko la kisasa wenye thamani ya shilingi milioni 705, Ujenzi wa shule ya Msingi wa  shilingi milioni 400, pamoja na kupatiwa Elimu bora ya ukusanyaji wa Mapato katika halmashauri ya Chalinze.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages