![]() |
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph akiwa katika eneo la Mto Nsanda ambapo kumekutwa Mifugoaina ya Ng'ombe zaidi ya 500 kwenye eneo hilo la hifadhi[Picha na Paul mathias] |
Na Paul Mathias
Mkuu wa wilaya ya
Mpanda Jamila Yusuph ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilaya ya Mpanda
kumusaka na kumukamata anaejiita Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nsanda Lushinge Lutamla Kijiji cha Katambike Kata ya
Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoa wa Katavi Nsimbo Kwa tuhuma za kuuza maeneo kwa
wafugaji na watu mbalimbali kwaajili ya makazi.
![]() |
Baadhi ya wananchi wa Kitongoji cha Nsanda waliouziwa maeneo na kuanza kufanya shughuli za ufugaji kwenye eneo la hifadhi[Picha na Paul Mathia] |
Mkuu huyo wa Wilaya amechukua hatua hiyo baada ya kubainika kuwa mwenyekiti huyo amekuwa akiuza Maeneo hayo Kwa wananchi yaliyo hifadhiwa na kuleta shida Kwa baadhi ya wananchi walionunua maeneo hayo.
‘’kuna mtu anaitwa lushinge Pande Lutamla alimaarufu anajiita kama balozi nielekeze kama serikali huyu mtu atafutwe ambae yeye anawaita wenzake na kuwauzia ekari 10 kwa shilingi 4,00000 zilizo hifadhiwa na amewaingiza wengine kwenye matatizo huyu lutamla atafutwe jeshi la polisi lipo lakini uongozi upo wa serikali ya katambike anafahamika’’
Akiwa katika Kijiji hicho hicho ameshuduhudia idadi kubwa ya mifugo ikiwa hifadhini hapo Hali iliyopelekea mifugo ya Ng'ombe na Mbuzi zaidi ya 520 ambayo imekamatwa katika eneo hilo na kuelekeza wafugaji hao kulipa faini kwa mujibu wa sheria za kiuhifadhi na kuondoka mara moja kwenye eneo hilo.
Katika hatua nyingine amewaonya watendaji wa serikali za Vijiji kutojipa mamlaka ya kuuza maeneo na kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali kinyume na utaratibu wa kisheria Hali ambayo imekuwa ikisabisha Migogoro baina ya watu wanao hamia maeneo hayo na Serikali
![]() |
Baadhi ya Ngo'mbe waliokutwa katika eneo la hifadhi kitongoji cha Nsanda Kijiji cha Katambike Kata ya Ugalla.[Picha na Paul Mathias] |
Mayunga Julias wa mkazi wa Ugalla ameeleza kuwa Balozi lushinge amekuwa akiuza Maeneo hayo Kwa wananchi na yeye tayari amenunua hekta kumi Kwa shilingi laki nne.
‘’haya maeneo alituuzia mzee Lushinge tulitoa laki nne tukapewa ekari 50 tulikuwa hatuandikishiani tulio uziwa maeneo haya ni wengi zaidi ya watu 50”
Amesema anaomba serikali kuwasaidia kwakuwa wameshanunua maeneo hayo na wanafanya kazi za kilimo na ugugaji katika maeneo hayo licha ya serikali kuwataka kuondoka kwenye maeneo hayo.
Kwa upande wake Paul Samweli ameeleza
kuwa amenunua maeneo hayo kutoka Kwa balozi huyo yapata miaka miwili Sasa na
hajui Cha kufanya baada ya kuambiwa maeneo hayo yapo hifdhadhini.
‘’kuna uongozi tulioukuta wa
kuteauliana kwamba kamati ya ugawaji wa Mashamba hususani zaidi ikaonekana mzee
Lushinge na kamati yake nikweli tulikuwa tunawakuta unapimiwa ekari 10 kwa
2,70000 nimekuja mwezi wa tisa mwaka jana nikanunua hapa” amesema samweli
Mara kadha serikali imekuwa ikisisitiza kulidwa Kwa Rasilimali za mazingira ikiwemo misitu na maeo oevu Kwa faida ya kizazi Cha Sasa na Baadaee.
kwa habari zaidi tembelea ukurasa wetu wa
kataviclub.blogspot.com