Mkuu wa Mkoa wa Katavi Comrade Juma Homera
Na Walter
Mguluchuma KTPC,Tanganyika.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Juma Zuberi Homera amewashauri viongozi wa Vjiji wa Kata tatu za Wilaya
ya Tanganyika Mkoani Katavi kutumia fedha wanazozipata
kutokana na kuuza hewa ya ukaa wazitumia kwa ajiri ya kuwakatia wananchi
wao Bima ya afya iliyoboreshwa CHF na wafungue maduka ya dawa
za binadamu kwenye vijiji vyao.
Wito huo kwa
viongozi wa vijji nane vya Kata tatu vinavyonufaika na kuuza hewa
ya ukaa aliutowa wakati wa kikao cha mkutano wa wadau wa utawala
bora na uhifadhi endelevu wa rasilimali za
maliasili katika Wilaya ya Tanganyika uliofanyika katika ukumbi wa
Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika .
Homera alieleza
kuwa kuna vijiji nane vya Kata za Katuma , Kasekese na Mwese ambavyo
mwaka jana vimenufaika kutokana na kuuza hewa ya ukaa yenye tani
82,000 baada ya kuwa wameingia mkataba na Carbon Tanzania .
Kwa kuwa viji hivyo
kwa mwaka jana wa 2020 waliweza kuuza hewa ya ukaa ukaa ya thamani ya
milioni zaidi ya 300 ambapo vijiji hivyo wameweza kuvitumia fedha hizo
kwa ajiri ya kufanyia miradi ya maendeleo kwenye vijiji vyao kama vile
kutengeneza madawati na ujenzi wa zahanati .
Hivyo
aliwashauri viongozi wa vijiji hivyo fedha ambazo watazipata kwa mwaka
huu kutokana na mauzo ya hewa ya ukaa ni vema wakazitumia pia kwa ajiri ya
kuwakatia wananchi wao Bima iliyoboreshwa ya CHF na wafungue maduka ya dawa
kwenye vijiji vyao ili wananchi wapate huduma kwa ukaribu zaidi kwa mwaka
mzima.
Aliwasisitiza
wahakikishe wanaendelea kutunza mazingira kwa nguvu zao zote kwani hewa
hiyo ya ukawa waliyouza haikupatikana kwa watu kuvuta sigara bali
imepatikana kutokana na utunzaji mzuri wa mazingira .
Vilevile
ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kutumia eneo lao la
msitu walilolihifadhi lenye ukubwa wa ekari 630,000 kwa ajiri ya
kuuza na wao hewa ya ukaa ili kuongeza mapato ya Halmashauri yao na pia
waweke mizinga ya asali ya kisasa na kuwa na mpango wa kujenga kiwanda
cha asali .
Alisema
kuwa biashara hiyo endapo itaendelezwa viziri itakuwa ni chanzokikubwa
sana cha mapato ya ndani kuliko hata mapato ya mazao.
Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Salehe Mhando Wilaya ya Tanganyika wanafarijika sana kufanya
kazi na Taasisi ambazo sio za kiserikali kama Tuunngane na nyinginezo
kwani zimekuwa na mchango mkubwa kweye Wilaya hiyo .
Awali wananchi wa
Wilaya hiyo walikuwa hawajuwi kama kuna biashara kama hiyo ya hewa ya ukaa
ambayo kumbe ni sehemuinayoongeza uchumi wa mwananchi na mapato katika
Halmashauri
Kwa msimu wa mwaka huu
2021 wanatarajia vijiji hivyo vinane vinatarajia kuuza hewa ya ukaa yenye
thamani ya shilingi milioni 500 hadi shilingi bilioni moja alisema Mhando
Mkurugenzi wa Taasisi
ya Tuungane Lukindo Hiza alieleza kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikifanya kazi
ya kujishughulisha na maswala ya utunzaji wa mazingira kwenye Wilaya hiyo na
maswala ya afya za watu.
Mafanikio
yaliyopatikana kwenye vijiji hivyo yametokana na ushirikiano wao na Halmashauri
ya Wilaya ya Tanganyika
Nae mwakilishi
wa Carbon Tanzania Frenk Kweka alisema kuwa vijiji hivyo vinauwezo wa kuzalisha
tani 280,000 ukilinganisha na tani 82 000 ambazo walizouza mwaka jana .
Alifafanua kuwa hapa
Tanzania mradi huu wa kuuza hewa ya ukaa upo katika Wilaya ya Tanganyika peke
yake na unamamufaa makubwa kwa wananchi na Serikali.
Utaratibu wa
fedha zinazotokana na mauzo ya hawa hiyo ya ukaa asilimia 90 huenda moja kwa
moja kwenye vijiji husika ambako fedha hizo hufanyiwa maamuzi na mkutano kuu wa
kijiji cha ajiri ya kufanyia mahitaji yaliopo ya kwenye kijiji hicho na
asilimia 10 huenda kwenye Halmashauri.