Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Katavi Faustine Maijo |
Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi
Katika kipindi cha miezi mitaa ya Oktoba hadi Desemba mwaka jana Takukuru Mkoa wa Katavi wamefanikiwa na kuokoa na kudhibiti jumla ya fedha Tshs 170,396,203 na wameanzisha utaratibu wa Mobile PCCB inayotembea kwa kutenga siku moja kila mwezi .
Fedha hizo ambao zimeokolewa na Takukuru na kuthibitiwa ni kwenye maeneo ya Mpate Saccos, chama cha ushirika Amos Kasekese , ukusanyaji wa ushuru ya pos na uvunaji wa magogo.
Kaimu Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Katavi Faustine Maijo alisema kuwa katika kipindi cha mwezi oktoba hadi Desemba mwaka jana wamefanikiwa kuokoa na kudhibiti jumla ya fedha Tshs 170,396,203 ambazo zimeokoewa na kudhibitiwa .
Aliyatajamaeneo waliyookoa fedha na kuthibiti kuwa ni maeneo yaMpate Saccos 550,000 Kasekese Amcos 62,974,520, ukusanyaji wa ushuru kwenye Halmashauri kwa njia pos tshs 54,757,060 na kiasi cha tshs 1,535,000 za wadaiwa sungu kwenye mikopo ya akina mama ,vijana na watu wenye ulemavu .
Katika ufatiliaji wa fedha za miradi ya Maendeleo wamefatilia miradi ya thamani ya Tshs 2,700,855,890 ambapo miradi hiyo ni ujenzi wa Hospitali katika Halmashauri ya Nsimbo , matumizi ya asilimia 10 kwa ajiri ya mapato ya ndani ya Halmashauri , ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Tanganyika pamoja na miradi ya maji na nyumba za walimu na zahanati .
Maijo alieleza kuwa katika kipindi hicho wamepokea jumla ya malalamiko 100 kati ya hayo 78 yalihusu vitendo vya rushwa na malalamiko 22 yalihusu makosa mengine .
Pia wanaendelea na uchunguzi wa watumishi watatu wa idara ya afya kituo cha Ilembo kilichoo katika Manispaa ya Mpanda wanatuhumiwa kuiba dawa za Serikali na kuomba na kupokea Rushwa kutoka kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa kwenye kituo hicho .
Maijo alieleza kuwa kuanzia mwezi januari mwaka huu wameanzisha utaratibu wa Mobile PCCB inayotembea kwa kutenga siku moja kila mwezi inayowafuata wananchi huko waliko kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero zao .
Lengo la kufanya hivyo
ni kuzidi kuongeza huduma zaidi kwa wananchi kwani wapo wamekuwa wakishindwa
kutowa taarifa za maswala ya Rushwa kutokana na kuishi mbali na ofisi za
Takukuru.