Agizo hilo limetolewa jana na Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa
wa Katavi,Faustine Maijo ofini kwake wakati wa uwasilishaji wa taarifa kwa
waadishi wa habari ya utendaji kazi wa kipindi cha mienzi mitatu tangu Oktoba
hadi Desemba,2020.
Maijo aliweka wazi
kuwa agizo hilo ni utekelezaji wa wito waliopewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Juma
Homera kutokana na matokeo ya ziara yake aliyoifanya katika wilaya za
Tanganyika na Mlele za kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Juma Homera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi aliagiza
Takukuru kufuatilia urejeshwaji wa fedha milioni 34 zinazotokana na watumishi
wa halmashauri hiyo 12 na wafanyabiashara watatu kujikopesha matofali ya
theruji 34,000 ya ujenzi wa hosptali ya wilaya ya Mlele kwa kujengea nyumba zao
binafsi huku baadhi ya majengo ya hosptali hiyo kusuasua kukamilika.
‘’…kuna matofali ambayo yalizuiliwa yasitumike baada ya
kuwa tumefanya uchunguzi na kuwa hayana ubora lakini hayo matofari mkurugenzi
aliwauzia watumishi wake kwa ajili ya kujengea majumba yao ,na wakati mkuu wa
mkoa anafanya ziara alikuta kunabaadhi ya watumishi hawajarejesha hizo
pesa…lakini hadi sasa ni milioni 11 zimesharejeshwa na tunasubili siku ya kumkabidhi
Mkuu wa Mkoa’’ alisema Kaimu Mkuu wa Takukuru.
Fedha milioni 11,Kaimu Mkuu wa Takukuru alifafanua kuwa
watamkabidhi Mkuu wa Mkoa huku kiasi cha fedha milioni 23 ambazo zilikuwa zimerejeshwa
pia na kuhifadhiwa kwenye akauti ya halmashauri hiyo zilitolewa na kutumiwa
kinyume na matumzi lengwa.
‘’mkurugenzi alikuwa safari Dar es salaam na ameagizwa
azirejeshe wakati wowote na Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Mlele anasimamia
zoezi hilo na wakati wowote fedha hizo zitarejeshwa ofisini’’ alisema Maijo.
Katika hatua nyingine Takukuru Mkoa wa Katavi kwa kipindi cha miezi mitatu imefanikiwa
kuokoa na kudhibiti Tshs 170,396,203.15 kwenye maeneo ya MPATE SACCOS Tshs 550,000/=,Idara ya Misitu
Tshs 1,000,000/= zinatokana na uvunaji wa magogo ya mbao kinyume cha utaraibu.
Aidha matumizi ya 10% za mapato ya ndani ya manispaa ya
Mpanda kwa ajili ya makundi maalumu Tshs
1,535,000/= zinazotokana na wadaiwa sugu kwenye vikundi vya akina mama,vijana
na walemavu,Chama cha Ushirika KASEKESE AMCOS Tshs 62,974,520/= zinazotokana na
wakandarasi wasio waaminifu waliowadhurumu wakulima wa pamba.
Vilevile Tshs 54,757,060/= zinazotokana na wadaiwa
sugu ambao walikuwa wakusanyaji wa
ushuru wa halmashauri. Sambamba na Tshs 10,792,000/= zimeokolewa na kurejeshwa
kwa Simon Maganga na wenzake ambapo ni malipo
ambayo Kampuni ya Modern Agrico ya Mkoa wa Rukwa inayojega barabara ya
Inyonga-Ilunde-Kishelelo-Kibo-Mwese-Lugonesi na Ifumbula ya kuchimba na
kusafisha mitaro.
Pia Takukuru inaendelea na uchunguzi wa watumishi wa afya
watatu wa kituo cha Afya Ilembo Manispaa ya Mpanda,Hussein Kimaro,Charles Daniel na Isack Muhigi kwa
tuhuma mbalimbali zikiwemo za wizi wa
madawa ya serikali pamoja na kuomba na kupokea rushwa.
Hata hivyo Takukuru inaomba wananchi kuzidi kutoa ushirikiano wa Taasisi hiyo kwa kutoa taarifa za vitendo vya rushwa
kupitia namba ya simu 113 au ujumbe mfupi wa maneno *113#.