MWENYEKITI WA HALMASHAURI NSIMBO ATOWA WITO KWA WAZAZI/WALEZI WASIOPELEKA WATOTO SHULE KUKIONA.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Mkoa wa Katavi Halawa Charles(amesimama) akiendesha kikao cha baraza la Madiwani.

 

Na John Mganga AHHWN HQ,Nsimbo.

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoa wa Katavi Mh Halawa Charles  Malendeja ametoa rai kwa wazazi na walenzi wa halmashauri hiyo kuacha visingizio na badala yake kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  wanahudhuria shuleni kwa wakati ili waweze kuendelea na masomo.

Malendeja ametoa rai hiyo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kwa ajili ya kujadili taarifa ya utekelezaji wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/21.

Ambapo amesema halmashauri haitosita kuchukua hatua za kisheria  kwa wale wataoshindwa kupeleka watoto shule kwa wakati.

Madiwani mbalimbali wakiwakilisha kata zao  wakiwa wakiendelea na mjadara  wa kupitia na kuchambua taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/21

Aidha Mwenyekiti Mlendeja amesisitiza kila mmoja kutimiza wajibu wake ambapo kwa wataalamu amewataka kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto ya uhaba wa madawati ili kuhakikisha kuwa watoto wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2021 wanaondokana na changamoto hiyo.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages