Na Walter Mguluchuma KTPC,Katavi.
Taasisi ya Tuungane imetowa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa vijiji nane vilivyoko katika katika Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi ya kuwajengea uwezo viongozi katika maswala ya utawala bora ili waweze kulinda na kuhifadhi vizuri maliasili na kutumia fedha vizuri zinazotokana na hewa ya ukaa.
Mafunzo hayo ya siku tatu yamefanyika kufuatia agizo alilolitowa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera Novemba mwaka jana wakati alipokuwa akikabidhi kiasi cha shilingi Milioni 250 kwa vijiji hivyo zilizotolewa na Carbon Tanzania zilizotokana na mauzo ya hewa ya ukaa tani 82,000.
Akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa utawala bora na uhifadhi endelevu wa rasilimali za maliasili wa Wilaya ya Tanganyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkurugenzi wa Programu ya Tuungane Lukindo Hiza alisema kuwa mafunzo hayo ya viongozi wa vijiji nane vilivyopo katika Kata za Katuma ,Kasekese na Mwezi yamefanyika kwa muda wasiku tatu
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi wa vijiji hivyo katika utawala bora ili waweze kulinda na kuhifadhi vizuri zaidi rasilimali na kuzitumia vizuri fedha zinazotokana na mauzo ya hewa ya ukaa kwenye vijiji vyao .
Katika mafunzo hayo Tuungane wameona fahari kubwa ya kuwa na wadau katika shughuli hiyo pia wamepata nafasi ya kusikia wadau wengine ambao wana uzoefu katika kufanya shughuli kwenye eneo hilo kama vile JGI na FZS.
Pamoja na kushughulikia matumizi bora ya ardhi katika vijiji 12 vya Wilaya hiyo Tuungane wanashughulikia afya za wananchi katika Wilaya hiii.
Pia utunzaji wa mazingira hasa ya mistu katika vijiji nane na kuviunga katika biashara ya hewa ukaa,upandaji wa miti misindano 2,350,000 katika maeneo ya Mwese, Lugonesi na Lwega.
Hiza alieleza kuwa pia wanafanya uvuvi endelevu katika Kata na vijiji vya pwani ya mwambao mwa ziwa Tanganyika na wameisha towa boti mbili za doria ,kilimo endelevu katika upandaji wa mazao ya kimkakati na wameisha towa kwa wakulima miche 1,100,000 za korosho bure.
Tuungane wanatarajia hivi karibuni kuliwezesha eneo la Lyamgoroka ambalo ni mapito ya wanyama wanaotoka kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi kwenda kwenye Hifadhi za Mahale na Gombe ambalo miti yake imekatwa ovyo sana liweze kukuza mistu kwa njia ya asili( Natural regeneration)
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Zuberi Homera alisema kuwa Tuungane wamekuwa ni wadau wakubwa wa uhifadhi wa mazingira katika Mkoa wa Katavi .
Alifafanua kuwa endapo biashara ya kuuza hewa ukaa katika Vijiji hivyo itaendelea vizuri itasaidiakuongeza pato la Halmashauri la mapato ya ndani kwani hadi sasa tani ambazo zimeuzwa bado ni chache .
Alisema manufaa ya utunzaji wa mazingira umeanza kuonekana kwenye vijiji hivyo kwani fedha walizozipata mwaka jana mwezi novemba kiasi cha shilingi milioni 250,000,000 zimesaidia kutengeneza madawati ya wanafunzi .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lugonesi Tarafa ya Mwese Mathias Kabade alisema kuwa wameanza kuona umehimu wa kutunza mazingira zaidi baada ya kuwa wameanza kupata manufaa ya kupata fedha za kuuza hewa ukaa.