Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tazania (UWT) Mkoa wa Katavi Fuljensia Kapama
Na Mwandishi Wetu KTPC,Katavi.
Serikali ya Mkoa wa Katavi imeombwa kuendelea na mapambano ya mimba za utotoni mkoani humo ili kujenga ustawi wa watoto kupata haki yao ya msingi ya elimu na kutimiza malengo yao kikamilifu ya siasa,utawala,uchumi na maendeleo yao binafsi na kwenye sekta mbalimbali za kitaifa.
Fuljensia Kapama ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Katavi ametoa rai hiyo kwa serikali ofisini kwake kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi (CCM) kitaifa.
Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa kama UWT wameendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi kupitia njia za radio,magongamano ya wanawake pamoja mikutano ya siasa huku wakiwaeleza athari ambazo zinaweza kujitokeza endapo vitendo vya ngono vitaendelea kwa watoto.
Licha ya kuiomba serikali kuendeleza juhudi za mapambono ya mimba za watoto,Wanawake mkoani humo wamehimizwa kuona umuhimu wa kuwalea watoto ili wafike umri wa kuzaa kwani kuzaa katika umri wa utotoni kuna athari kubwa.
" hakuna mwanaume ambaye anayekubali kulea mtoto ambaye ni wamwanaume mwenzie...hivyo wakinamama tulee na kuwatunza watoto wetu na endapo tutaona watoto wanatushinda kunavyombo ambavyo vinavyohusika kama vile polisi,maendeleo ya jamii ambavyo vyote vinaweza kutusaidia"alisisitiza mwenyekiti huyo.
Aidha Fuljensia aliwataka wanawake kuachana na mila potofu za kuongopa kuwapatia elimu ya afya vijana kwa athari endapo mtoto atapata ujauzito atazaa kwa kupasuliwa,kuzaa mtoto ambaye hajakomaa kutokana na kuzaliwa na mtoto mwenzie na kwa wakati huo huo kufariki mama pamoja na mtoto.
Athari zingine ni kuwa malezi ya mtoto huyo aliyezaliwa yatakuwa shinda kutokana na kuwa amezaliwa na mtoto mwenzie na mzingo huo kuangukia kwa wazazi au walezi wa mtoto aliye aliyezaa kabla ya wakati wake.
Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Katavi Asha Juma.
Katibu wa UWT Mkoa wa Katavi Asha Juma kwa upande wake amebainisha kuwakuelekea maadhimisho ya CCM kitaifa,Umoja huo unaendelea kuhamasisha wanawake wote kushirikishwa katika vyombo vya maamuzi kuanzia serikalini za mitaa hadi juu.
Aisha amesema kuwa tangu kuzaliwa kwa CCM wanawake wamepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na wanawake kushiriki bega kwa bega na wanaume katika ulizi wa taifa,wanawake kushiriki katika suala la uzalishaji mali,wanawake kumiliki mashaba na ardhi.
Mafanikio mengine ni wanawake kuteuliwa sawa na wanaume katika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali sambamba na wanawake kuendelea kupata elimu sawa na watoto wa kiume.
Aidha wanawake wameendelea kuhamasishwa na kuelimishwa kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kama SACA,VIKOBA na SACCOS na kuvisajili ili wapewe mikopo ya kuendeleza biashara zao waweze kujikwamua kiuchumi kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Vilevile kutokana na mkoa wa Katavi kuwa na fursa za kiuchumi,kuelekea maadhimisho ya miaka 44 ya CCM Katibu huyo ametoa wito kwa wanawake kujenga tabia ya kujiamini kuwa wanaweza na wasikate tamaa,kuendeleza ushirikiano kati yao na wanaume katika ujenzi wamaendeleo pamoja na wanapokutana na vikwazo na maswali wapambane na kutafuta ufumbuzi ili kufikia malengo yao.
Mwenyekiti wa chama chama Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi Ndg Beda Katani.
Beda Katani,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi amesema kwenye maadhimisho hayo wanatarajia kufanya mambo ya kijamii kama kuchangia damu na kutembelea vituo vya kulelea watoto yatima.
Mwenyekiti huyo ameweka wazi kuwa licha ya hatua kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM ya kuboresha miundombinu ya barabara ya kujenga kwa kiwango cha lami,kutolewa elimu bure ni baadhi ya mafanikio ambayo wananchi waendelee kukiamini chama hicho