Na Walter Mguluchuma KTPC ,Katavi
Baraza la Madiwani wa Manispaa
ya Mpanda na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
wamepitisha mapendekezo ya bajeti ya Maendeleo ya kipindi cha mwakaa
2021na 2022 huku Mamispaa ya Mpanda ikiwa imependekeza Bajeti ya zaidi ya
Bilioni 21 na Halmashauri ya Tanganyika kiasi cha zaidi ya Bilioni 33.3 .
ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.8
Akisoma taarifa ya mapendekezo
ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Afisa Mipango wa Halmashauri
hiyo Doto Kwigema alieleza kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2021/
2022 Halmashauri hiyo imependekeza kutumia bajeti ya kiasi cha Tshs
bilioni 33,,336,597.500 ikiwa ni ongezeko la asilimia
7.8 la bajeti ya msimu uliopita bajeti ilikuwa ya kiasi cha zaii ya
shilingi Bilioni 30 .
Kwa upande wa makusanyo ya
mapato ya ndani wamepanga kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni
5,712,006,000 ikiwa na ongezeko la asilimia 44.37 ya bajeti
ya msimu uliopita ya kiasi cha zaidi ya shilingi
Bilioni 3.1.
Alifafanua kuwa hadi Desemba
mwaka jana kwa upane wa mapato ya ndani ya kiasi cha shilingi
Bilioni zilikuwa zimekusanywa 2. 1 ikiwa ni sawa na asilimia
68 ya mapato yao ya ndani hivyo kwa upane wa makusanyo ya 2020/ 2021
wanakwenda vizuri hivyo hadi kufikia june 30 mwaka huu watakuwa wamekusanya kwa
asilimia 100.
Alifafanua kuwa ongezeko la bajeti ya
mapato ya ndani yametokana na ubunifu wa ukusanyaji wa mapato ya
ndani kwa kubuni vyanzo mbalimbali kama vile mrahaba wa
hewa ya ukaa unatarajiwa kuingiza kiasi cha Bilioni 1.2 ushuru wa mbao , vivutio
vya utalii na vinginevyo
Kwigema aliliambia Baraza hilo
la madiwani kuwa waliopitisha ni mapendekezo tuu yatakuwa ni matumizi
mpaka hapo Bunge litakapo limepitisha mapendekezo hayo hivyo inaweza ikawa kama
walivyopendekeza au ikapungua kutoka na jinsi Bunge litakavyo pitisha
mapendekezo hayo ya bajeti .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tanganyika Hamad Mapengo alisema kuwa pamoja na kuwa
wamependekeza makusanyo hayo wanaweza kukusanya zaidi endapo tuu watafanya kazi
kwa ushirikiano hivyo ni vema wakafanya kazi ya ziada katika
kukusanya mapato hayo ili wafikie lengo la kulivuka kwani ongezeko la asilimia
44.37 sio ndogo .
Alisema kuwa mapendekezo
hao ya bajeti yaliyosomwa kwenye baraza hilo yamepitia kwenye kamati
za madiwani na kwenye bajeti hiyo yapo mapendekezo
yaliyotolewa na kuingizwa baada ya kutolewa na kamati ya ushauri ya
Wilaya kwenye maeneo mbalimbali .
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo
John Rojas alieleza kuwa Bajeti hiyo ya vHalmashauri ya
Tanganyika ni mchakato ulioanzia kwenye kazi ya Jijiji hivyo
imegusa kila hitaji la kila sehemu la wananchi katika Halmashauri ya Tanganyika
.
Alibainisha kuwa wanayo kazi
kubwa ya kukusanya mapato lakini kutokana na jitihada walizo nazo wanao uhakika
wa kuvuka lengo la oil kuzidi kuwaletea wananchi wao maendeleo zaidi na kwa
kutambua Wilaya hiyo ni kubwa na alitowa mfano wa matumizi ya mafuta ya
gari wanayotumia wao kwa wiki moja alisema ni sawa na matumizi ya miezi mitatu
kwa baadhi ya Halmashauri za Mkoa huu.
Kwa upande wa Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda Baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo limepisha
mapendekezo ya bajeti ya 2021/2022 ya kiasi cha shili Bilioni zaidi ya shilingi
Bilioni 21.5 huku mkusanyo ya ndani yakiwa ni kiasi cha zaidi ya bilioni mbili
.
Afisa Mipango wa Manispaa
ya Mpana Waza Benjamini alieleza kuwa kati ya fedha hizo
zaidi ya bilioni 19 wanatarajia ni fedha ambazo zitatoka Serikalini na
fedha nyingine ni za mapato ya ndani .
Alisema katika kuhakikisha
wanafikia malengo ya ukusanyaji wameweka mikakati mbalimbali ya kuziba
wizi wa upotevu wa mapato kwa kwani wataongeza mashine za ukusanyaji
fedha kwa njia ya posi .
Meya wa Manispaa ya Mpanda Haidari
Sumry alisema kuwa kumekuwa na tatizo la miradi ya maendeleo kutokwisha kwa
wakati kutokana na ucheleweshaji wa fedha za maendeleo za kutoka Serikali kuu
ambazo zimekuwa hazifiki kwa wakati .
Katika kuhakikisha wanafikia malengo
wamepanga kuwahamasisha wawekezaji ili waje wafungue viwanda ili kuongeza
thamani ya mazao ghafi ili mazao yaweze kuuzwa kwa bei kubwa