Na Zilper Joseph KTPC,Mpanda.
Wakulima wa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wamehamasishwa
kuendeleza kilimo cha ufuta ili kujiongezea kipato kutokana na zao hilo kuwa na
soko kubwa duniani kote
Ushauri huo umetolewa na Mratibu wa Programu ya Kilimo cha Mbegu
za Mafuta kutoka kituo cha utafiti wa kilimo TARI Naliendele bwana Joseph
Nzunda wakati akizungumza na wakulima wa ufuta wa halmashauri ya Nsimbo na
Manispaa ya Mpanda wilayani Mpanda mkoani Katavi
Aidha amewasisitiza juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo cha
ufuta ili kuweza kupata mavuno ya kutosha
Akieleza lengo la ziara yao mkoani katavi bwana nyunda amesema
ni pamoja na kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo cha ufuta na kuongeza
kuwa kutokana na hali ya hewa ya mkoa wa katavi wakulima wanaweza wakapata
mavuno mengi na kubadilisha kabisa hali ya uchumi wa familia zao
Kwa upande wao wakulima walieleza changamoto kadhaa ikiwemo zao
hilo kushambuliwa na magonjwa mbalimbali likiwemo shambani
Akijibu changamoto hizo mtafiti wa mbegu za mafuta kutoka TARI
Naliendele bwana Athanas Minja amesema ni vizuri mkulima akapiga dawa mapema
pindi anapoona wadudu wameanza kushambulia
Aidha ili kudhibiti wadudu katika shamba , amewataka msimu wa
kwanza kupanda ufuta na msimu unaofuata kupanda zao jingine ili kuondoa wadudu
wanaoshambulia ufuta
Awali Afisa ugani wa mkoa wa katavi Faridu Abdallah amesema kwa
msimu uliopita wakulima wa ufuta walipata zaidi ya shilingi bilioni 5 kutokana
na kuuza zaidi ya tani 3,000 za ufuta