DC JAMIRA AKAGUA MIUNDOMBINU YA MADARASA NA MADAWATI SHULE ZA MSINGI

 

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Jamira Yusuph (wa kwanza kutoka kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda,Michael Nzyungu (wa pili kutoka kulia).


Na Mwandishi Wetu AHMM ,Mpanda.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Mhe.Jamira Yusuph akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo amekagua hali ya mahudhurio  ya wananfunzi darasa la awali pamoja na darasa kwanza.

Mahudhurio ya wanafunzi amekagua  katika shule za msingi zilizopo Manispaa ya Mpanda .

Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi,Michael Nzyungu (ametangulia  mbele)akiwa na baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mpanda katika ziara iliyoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Jamira Yusuph ya kukagua mahudhurio ya wanafuzi wa darasa la awali na la kwanza sambamba na kukagua miundombinu ya madarasa na madawati

Jamira Yusuph ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda vilevile amekagua miundombinu ya madarasa pamoja na madawati  huku akimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,Michael Nzyungu  kwa namna anavyojitahidi kukamilisha miundombinu ya madarasa na kwa jinsi anavyojitahidi kutengeneza madawati na kuyasambaza mashule ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kukaa chini  inayosababishwa na ongezeko la wanafunzi.

Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulizni na usalama ya wilaya ya Mpanda wakiwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule za msingi mansipaa ya Mpanda.

Katika ukaguzi huo Mkuu wa Wilaya ameridhishwa na namna wazazi walivyowajibika kwa kuwaandikisha watoto wao ili waanze  masomo. 

 Kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiandikisha kuanza darasa la awali na darasa la kwanza Mkuu wa wilaya  amewataka wazazi na jamii nzima kuanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi kufikia usawa wa lenta kwa  kuchangia na kujitolea nguvu zao na baadae serikali imalizie ili watoto waendelee kujifunzia kwenye mazingira rafiki

 

 


Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages