DENI LA TAIFA NCHINI LAONGEZEKA KWA ASILIMIA 7.6


 Na Mwandishi Wetu KTPC.

Ongezeko la deni la Taifa nchini Tanzania limefikia kiasi cha trilioni 59 hadi kufikia mwaka 2020 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 7.6 ikilinganishwa na shilingi trilioni 54.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2019, huku Bunge likitoa ushauri liwe himilivu.

Kati ya kiasi hicho deni la ndani limefikia sh trilioni 16.2 na deni la nje sh. Trilioni 42.8.

Ongezeko la deni limetokana na ukopaji kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Gazeti la Nipashe nchini Tanzania limeripoti

Hayo yamebainishwa na Sillo Baran Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti alipokuwa akiwasilisha taarifa kuhusu tathimini ya utekelezajiwa mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2017 mpaka 2020/2021.

Ingawa deni hilo ni himilivu kwa viashiria vyote muhimu serikali imeshauriwa ione haja ya kujipima uhimilivu wakekwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani.

Kwa mujibu wa tathimini ya uhilimivu wa deni imeonesha kuwa deni la serikali ni himilivukatika kipindi cha muda mfupi , wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo unaokubalika kimataifa kwa viashiria vyote muhimu.

Kamati ya Kudumu ya Bunge na Bajeti imeishauri katika maoni ya jumla kutafuta njia ya kupunguza kukopa katika soko la fedha la ndani ili kuziba nakisi ya bajeti kwa kupitia dhamana ya serikali na hati fungani.

Badala yake, serikali ijikite zaidi katika kuongeza matumizi ya mikopo inayojidhamini ni yenyewe.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages