JPM HANA MPANGO WA KUBAKI MADARAKANI

Rais wa Jamuhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt John Magufuli

 Na Mwandishi wetu KTPC.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole amesema kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli hana mpango wa kuongeza muda wa kukaa madarakani.

Mbunge wa Konde, Khatib Said Haji kupitia chama cha ACT-Wazalendo bungeni leo aliibua suala hilo akikosoa wabunge wawili wa CCM ambao walitoa hoja ya kutaka Rais Magufuli kuongezewa muda na Polepole kujibu hoja zao.

Akitoa taarifa kwa mbunge huyo wa ACT, Polepole amesema kuwa Rais hataongeza muda wowote.

“Masuala ya Chama cha mapinduzi hujadiliwa kwenye vikao vya chama , hapa bungeni wabunge wana uhuru wa kuzungumza lakini kinachozungumzwa humu ndani hakiathiri msimamo wa Chama cha Mapinduzi ambao tumeshautoa, Rais hataongeza muda,” ameeleza Polepole.

Mjadala wa kuongeza muda wa rais madarakani umerejea tena hivi karibuni baada ya wabunge wawili wa CCM kuchangia Bungeni.

Awali, katika muhula wake wa kwanza, Rais Magufuli alipuuzia mapendekezo hayo kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge lililopita akiahidi kutoongeza hata dakika moja muda wake wa kuondoka madarakani utakapofika.

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages