DC: MLELE AHIMIZA UTUNZAJI MAZINGIRA KWA VITENDO


Mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga akifungua mkutano wa kawaida wa Mwaka Jumuiya ya watumia Maji ngazi ya Jamii zilizopo chini ya Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Ruwasa  halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi


Na Paul Mathias,Mpimbwe

Jamii katika halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele imeaswa kuongeza Juhuhudi katika kuhifadhi mazingira ikiwemo upandaji wa miti ili kukabiliana na Mabadilko ya hali ya hewa ikiwemo ukame.

Viongozi wa kamati za Watumia maji Ngazi ya Jamii Pamoja na Viongozi wa Vijiji wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Jumuiya za watumia Maji ngazi ya Jamii halmshauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi.

Jamii katika halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele imeaswa kuongeza Juhuhudi katika kuhifadhi mazingira ikiwemo upandaji wa miti ili kukabiliana na Mabadilko ya hali ya hewa ikiwemo ukame.

Akifungua mkutano wa Mwaka wa Jumuiya za watumia maji ngazi ya Jamii zilizo chini ya wakala wa usambazaji Maji na usafi na mazingira vjijini Ruwasa Halmashauri ya Mpimbwe mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema jamii lazima iendelee na utaratibu wa Kupanda miti ili kuhifadhi vyanzo vya Maji.

 Majid ameikumbusha jamii na wanachi kwa ujumla kuendelea kuhifadhi mazingira kwa kupata miti ili kuepukana na Janga la ukame.

Kaimu Meneja Ruwasa Mkoa wa Katavi Mhandisi Yeremia akitoa neno kwa washiriki wa kikao cha mwaka cha Jumuiya za watumia Maji halmashauri ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi
‘’tunakwenda kwenye Msimu wa Ukame lakini lazima tusimamie utunzaji wa Mazingira hasa upandaji wa Miti tunakazi kubwa ya kutunza Mazingira ili maji yapatikane sababu hali ya upatikanaji wa Maji si nzuri sana’’

Amesema kuwa ili huduma za upatikanaji wa Maji ziendelee lazima kwenda sambamba na zoezi la upandaji miti kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa Maji ni Mhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu katika shughuli mbalimbali.

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mlele Charles Mengo amesema Ruwasa halmashauri ya Mpimbwe inaendelea kutekeleza miradi mbalmbali ya Maji kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi

Wajumbe waliohudhuria kikao hicho wakichangia mambo mbalimbali kuhusu huduma ya Maji 
‘’kwa mwaka fedha wa 2022/2023 jumla ya Miradi Mitatu inaendelea ikiwa ni pamoja na Mradi wa Maji safi na salama Majimoto Usevya ,Mradi wa Maji Mwamatiga,vilolo na Mkwajuni na ujenzi wa Tank la Maji lenye ujazo wa lita milioni moja katika kijiji cha Mamba ‘’amesema Mengo

Amefafanua kuwa halmashauri ya Mpimbwe imebahatika kupata chanzo cha Maji cha Mto Mamba chenye uwezo wa kuhudumia vijiji 18 ambavyo kati ya hivyo vijiji 10 vinapata huduma ya maji huku vijjiji 8 utekelezaji wa Miradi ukiwa unaendelea

Masanja Mongela Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikuba akichangia hoja katika kikao hicho ameishukuru Ruwasa kwa kufikisha Huduma ya Maji katika kijiji hicho na kuomba miundo mbinu iliyofungwa kwenye kijiji chake kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi.

‘’nashurukuru Magati ya maji yamenifikia inagawa hayatoshi hasa kwenye vijiji vilivyokuwa vinatumia Maji katika mto Higu Ruwasa nawaomba mniongezee magati amesisitiza ‘’

Kwa upande wake Izilaeliti Mwiga amesema serikali ichukue hatua ya kukilinda chanzo cha Maji cha Mto Mamba ili kiendelee kuwahudumia wananchi kwani kuna baadhi wamekuwa wakikivamia chanzo hicho kwa kufanya shuguli mbalimbali.

‘’ule mto ukiufatilia chanzo chake mpaka sasa hivi kilisha vamiwa na wakulima kule juu tulishaongea mara nyingi kwenye hivi vikao serikali ichukue hatua ili kunusuru chanzo kile’’

Ili kuhakikisha wananchi waishio maeneo ya Vijijini wanapata huduma ya Maji serikali iliunda chombo maalumu cha wakala wa usambazaji Maji na usafi wa Mazingira Vijijini Ruwasa ili kuhakikisha huduma ya maji maeneo ya Vijijini inapatikana kwa kwa ufasaha.

 kwa habari zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu wa

kataviclub.blogspot.com

Search This Blog

CHAGUA HABARI

Pages